UVCCM MKOA WA ARUSHA WATOA SIKU 14 KWA WALE WOTE AMBAO HAWAJALIPA KODI ZA MAJENGO YAO,NA WALE WALIOJIMILIKISHA MALI ZA UMOJA HUO
mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya akiwa anaongea na waandishi wa habari
mwenyekiti wa UVCCM wialaya ya Arumeru Boniface Mungaya akichangia jambo katika mkutano huo ambapo alisema kuwa watakuwa bega bega viongozi hao kuakikisha mali za umoja huo silizotaifishwa zitarudishwa ,wakwepa kodi watalipa au kufukuzwa na maduka yote yanapangishiwa wananchi wa CCM ili wanufaike
Kamanda wa UVCCM Philemoni Monaban akiongea na waandishi nae alisema kuwa anawaunga mkoano vijana hawa na atakuwa nao bega kwabega
mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya akiteta jambo na kamanda wa UVCCM
Na Woinde Shizza,Arusha
UMOJA wa vijana mkoa wa Arusha UVCC, umetoa siku 14 kwa wapangaji wote waliokiuka kulipa kulipa kodi za pango la miradi ya umoja huo na endapo watakaidi amri hiyo ya kulipa kodi hizo hatua kali zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani.
Akiongea na vyombo vya habari Mara baada ya kumalizika kwa kamati ya utekelezaji mapema katibu wa Umoja huo Ezekieli Molel alisema kuwa wapo baadhi ya viongozi ambao wanahusika kuhujumu miradi ya Umoja huo na kisha kulipwa kama wamiliki halisi wa majengo na miradi ya Umoja huo.
Alisema kuwa miradi inatakiwa kuingiza kiasi cha milioni zaidi ya 20 kwa mwezi lakini kitu cha ajabu miradi hiyo inaingiza kiasi cha milioni tatu pekee kwa mwezi.
Alidai kuwa kinachotokea ni kwamba wapo wapangaji ambao wanalipa kodi kwa kiasi cha 5000 kwa mwezi kwa kuwa wanafahamina na wamiliki waliojiandikishia mkataba hali amabyo inawafnya wengine kujinufaishia juu ya migongo ya umoja huo.
"Tunalagaiwa sana alafu hawa wapangaji wetu wanatupa shida alafu Mkuu wa mkoa anawatetea baadhi yao kwa kusema kuwa tuwaache kweli jamani tupokee kodi 5000 hatukubali kabisa na wengine wamekaa muda mrefu lakini hawalipi kweli ni haki hapana atutakubali tutakula nao sahani moja"aliongeza molel
Kwa upande wake mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya alisema kuwa kuna taarifa zinaonesha kuwa aliyewahi kuwa katibu wa Umoja huo ambaye ni mfaume kizigo(naibu katibu Mkuu bara)alihusika kwa namna moja kudidimiza uchumi wa umoja huo.
Kutokana na hali hiyo mwenyekiti huyo alimtaka naibu katibu Mkuu kurudi Arusha na kisha kuweza kuangalia makubaliano ambayo aliingia na wapangaji wakati alipokuwa katibu wa vijana mkoani hapo "kuna vigogo ambao kwa kuwa wana majina ndani ya chama wanarubuni mali
za chama kabisa sasa hatutakubali kabisa hata kama wapo ngazi za juu ni lazima tuhakikishe tunawatoa"aliongeza Ole sabaya
Kutokana na hilo alisema wametoa siku 14 kwa wapangaji ambao wanahujumu miradi ya chama hicho kujisalimisha na kisha kulipa madeni yote na endapo kama watashindwa kufanya hivyo watafakisha mahakamani.
Aidha aliongeza kuwa kama kunampangaji yeyote aliyepangisha duka alilokabidhiwa na umoja wa vijana nae akapangisha kwa mtu mwingine yeyote hata kama ni kiongozi ndani ya chama amekosa sifa za kuwa mpangaji kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba na toka sasa hatambuliki tena .
Ole Sabaya aliongeza kuwa wao kama umoja wa vijana mkoa wa Arusha wanalaani vikali matamshi ya mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema na viongozi wake kwa ujumla kwa kuingilia mamlaka halali ya mkuu wa wialya ya Arusha mjini Mrisho Gambo ya kutaka kujua uhalali wa fedha wanazolipwa madiwani kinyemela huku wananchi wa jiji wakiendelea kupata dhiki ya maji ,afya pamoja na miundo mbinu
Walimtaka mkuu wawilaya aendelee na kazi bila ya woga wala hofu huku akimfundisha mbunge huyo kufata mipaka ya kazi yake na kukumbuka kwamba kazi aliy9oomba sio ya kunufaisha matumbo ya madiwani wake bali ni ya kuwapunguzia wana nchi wa Arusha ukali wa maisha.
Katika hatua nyingine akiongea kwa njia ya simu naibu katibu mkuu wa UVCCM taifa, mfaume kizigo alisema kuwa tuhuma hizo ni za uongo kabisa nayeye hausiki na mkataba wowote kwani kwa mujibu wa sheria za CCM mikataba yote inafanyika na kuna kuwa na uwazi Alidai kuwa hana mali yoyote ambayo ameihujumu na hivyo hao vijana kama wangekuwa na malalamiko basi wangeyafikisha kwenye uongozi ngazi za juu.
Hataivyo jitiada za kumtafuta Mkuu wa mkoa wa Arusha daudi Ntibenda zinaendelea.
0 comments:
Post a Comment