WAZIRI NCHINI SWEDEN AJIUZULU BAADA YA KUENDESHA GARI HUKU AKIWA AMELEWA
Waziri kijana kuliko mawaziri wote waliowahi kuteuliwa nchini Sweden, Aida Hadzialic, amejiuzulu baada ya kukutwa akiendesha gari huku akiwa na kiwango kikubwa cha pombe mwilini.
Waziri Hadzialic, 29, ni Waziri wa Elimu ya Juu katika serikali ya mrego wa kati wa kushoto na ni waziri wa kwanza Muislam nchini Sweden.
Hadzialic amesema kitendo chake hicho cha kuendesha gari huku akiwa amelewa ni kosa kubwa katika maisha yake.
Hadzialic, ambaye alihamia nchini Sweden akiwa na umri wa miaka 5 akitokea Bosnia-Hercegovina, alikunywa glasi mbili za wine kabla ya kusimamishwa katika daraja linalounganisha Denmark na Sweden.


0 comments:
Post a Comment