GUARDIOLA AANZA NA USHINDI EPL DHIDI YA SUNDERLAND
Kocha Pep Guardiola amepata ushindi wake wa kwanza baada ya Paddy McNair kujifunga dakika za mwisho na kuipatia Manchester City ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Sunderland inayonolewa na David Moyes.
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Uingereza Sergio Aguero aliipatia Manchester City goli kwa mkwaju wa penati kufuatia kuchezewa rafu Raheem Sterling na Patrick van Aanholt, na kuifanya City iongoze.
Hata hivyo Guardiola, a mbaye alimuweka benchi kipa wa timu ya taifa ya Uingereza Joe Hart alijikuta akifungwa goli la kusawazisha na Jermain Defoe. Goli la City la pili lilifungwa na McNair ambaye alijifunga kwa kichwa.
Jermain Defoe akiachi shuti lililojaa wavuni na kuandika goli
Paddy McNair akipiga mpira wa kichwa na kujifunga goli
0 comments:
Post a Comment