Saturday 3 September 2016

BODI YA NDC YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

jag1
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje akiongea na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Maendeleo  (NDC) wakati akiizindua  Jijini Dar es Salaam, ambapo ameitaka bodi hiyo kushika miradi mikubwa ya uwekezaji na kuhakikisha inairudisha katika hali yake ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati kupitia uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda.
jag2
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa Maendeleo (NDC) Dkt. Samweli Nyantahe akiongea na wajumbe wa bodi hiyo na kuwataka kujipanga ili kutekeleza majukumu kama ilivyoelezwa na  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje(kulia) ikiwemo kuanza kusimamia miradi ya Shirika hilo na kiuhakikisha inaanza kutekelezwa
jag4
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje(kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa Maendeleo (NDC) Dkt. Samweli Nyantahe nyaraka mbalimbali zitakazomuongoza katika utendaji kazi.
jag5
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Maendeleo  (NDC) mara baada ya kuizindua  Jijini Dar Es Salaam. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WAZIRI wa Viwanda ,Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema Shirika la  Taifa Maendeleo ya Viwanda (NDC) ndio injini ya kushikiria sekta ya viwanda na hivyo inatakiwa kuhakikisha ndani ya miaka minne inakuwa  viwanda hata vitatu katika kuweza kufikia uchumi wa kati.
Mwijage ameyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa BAodi mpya ya Wakurugenzi NDC, amesema kuwa bodi lazima ifanye kazi kuhakikisha inashikiria viwanda vikubwa ambayo vitafanya taifa kuwa na maendeleo ya kiuchumi kutokana miradi iliyopo chini ya NDC.
Amesema kuwa mradi wa kwanza ni ule wa Liganga na Mchuchuma unatakiwa kufutika midomoni  mwa watu kwa kuanza kuzalisha kutokana na muda mrefu umekuwa ukizungumzwa.
Mwijage amesema kuwa  kutokana bodi hiyo kuwa na watu wa kila sekta muhimu hivyo wanahitaji kukutana mara kwa mara hata bila kulipwa posho ili mambo yeande na kuleta tija kwa taifa.
Amesema kuwa miradi mikubwa ikikamilika nchi itakuwa imepiga hatua kimaendeleo na kuweza kufikia uchumi wa kati  wa viwanda vyenye kwa wananchi.
Nae Mwenyekiti wa bodi wa NDC,  Dk, Samwel Nyantahe amesema kuwa watafanya kazi kwa karibu na wizara ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi yote na kuweza kuanza kufanya kazi kwa nguvu.
Amesema Rais Dk. John Magufuli amemuamini hivyo watatimiza wajibu kwa kushirikiana na bodi hiyo katika sekta ya viwanda.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA