Saturday 3 September 2016

SERIKALI YASISITIZIA AZMA YAKE YA KUHAMIA DODOMA

DM1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia muonekano wa Jengo jipya la makazi ya Mhe Waziri Mkuu lililopo Mlimwa Dodoma wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana.
DM2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagam (katikati) akipewa maelezo ya eneo la Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim kutoka kwa Mtaalam wa Masuala ya Ujenzi Bw. Keffa Chana alipofanya ziara ya kukagua makazi haya Septemba 02, 2016 Mlimwa Dodoma.
DM3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa baadhi ya maagizo kwa viongozi wa Serikali wakati wa ziara yake katika Jengo jipya la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  wa Dodoma Septemba 2, 2016 wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Jordan Rugimbana.
DM4
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia muonekano wa jengo jipya la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alipofanya ziara yake tarehe 02 Septemba, 2016 Dodoma.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU) 
Na. MWANDISHI WETU.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (mb) amesisitiza kuwa dhamira ya Serikali kuhamia Dodoma ipo palepale ndani ya kipindi cha miaka minne hatua kwa hatua.
Akizungumza na waandishi wa habari Septemba 2, 2016 wakati wa ziara yake eneo la Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim yaliyopo Mlimwa Dodoma, Waziri Mhagama alisema “Watanzania wawe na amani, dhamira yetu iko vizuri na kama Mhe. Rais alivyosema na tunawahakikishia kwamba ndani ya kipindi hicho sisi tumeshajipanga kuhamamia mkoani Dodoma hatua kwa hatua”.
Waziri Mhagama alieleza kuwa shughuli za maendeleo hazitosimama kwa kuzingatia mipango iliyopo na bajeti ya Serikali, “Niwatoe wasiwasi kwamba mipango yote ya maendeleo haitosimama na shughuli zote za maendeleo hazitozuiwa na ujio wa Serikali mkoani Dodoma zitafanyika kama zilivyopangwa na tutaendelea kuyafanya hayo kwa kuzingatia Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 Ibara ya 151 tumesema tunahamia Dodoma na tutafanya hivyo”.Alisisitiza Mhagama
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana ameahidi kutekeleza usimamizi wa maagizo ya Waziri ili kukamilisha ujenzi wa barabara kwa wakati “kwa upande wa mkoa kazi iliyobaki ni kuhakikisha kuwa ujenzi  wa barabara unakamilika na tutakutana na Wakala wa Barabara (TANROADS), Mamlaka ya Ustawishaji Mji (CDA) na Manispaa ili kuona shughuli hii tunaifanyeje kwa kutekeleza maagizo hayo ikiwa ni sehemu ya majukumu ya mkoa.”
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana alimshukuru Waziri Mhagama kwa kutembelea maeneo ya makazi mapya ya Mhe. Waziri Mkuu na Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,”Namshukuru Mhe. Waziri Mhagama, Manaibu Waziri na Ofisi yote ya Waziri Mkuu kwa ziara hii na kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu.” 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA