Monday 19 September 2016

KILIMANJARO QUEENS YAIFUMUA 4-1 UGANDA NA KUTINGA FAINALI CHALLENGE


TIMU ya taifa ya Tanzania Bara ya wanawake, Kilimanjaro Queens imeingia fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, Uganda leo Uwanja wa Ufundi, Njeru mjini Jinja.
Kili Queens sasa itamenyana na Kenya, ambayo imeifunga 3-2 Ethiopia katika Nusu Fainali nyingine leo. Mabao ya Tanzania Bara leo yamefungwa na Donosia Daniel dakika ya sita, Mwanahamisi Omari 'Gaucho' dakika ya 17, Stumai Abdallah dakika ya 31 na Asha Rashid 'Mwalala'.

Fainali ya CECAFA Challenge ya kwanza ya wanawake inatarajiwa kufanyika Septemba 20, ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA