Sunday 18 September 2016

LEICESTER YAIFUMUA BURNLEY 3:0, MGENI ISLAM ATUPIA 2

Mchezaji mpya wa Leicester City aliyesajiliwa kwa rekodi Islam Slimani amecheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu na kuifungia timu yake magoli mawili katika ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Burnley.

Mshambuliaji huyo alifunga goli lake la kwanza mnamo dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza kwa kichwa kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Christian Fuchs.

Slimani alifunga la goli la pili kwa kichwa mara tu baada ya kuanza kipindi cha pili kabla ya Ben Mee kujifunga la tatu baadaye wakati akijaribu kuokoa mpira.
       Islam Slimani akiwa juu angani baada ya kuupiga mpira wa kichwa uliojaa wavuni
                Beki Ben Mee akijifunga goli wakati akijaribu kuokoa krosi ya Mahrez 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA