Saturday 17 September 2016

LIVERPOOL YAWADUWAZA MASHABIKI WA CHELSEA KWA KIPIGO CHA 2:1 KATIKA UWANJA WA STAMFORD BRIDGE


Chelsea keeper Thibaut Courtois dives in vain as Lovren's shot screams past him to hand Liverpool the lead
Beki Dejan Lovren akiiandikia Liverpool bao la kwanza
Utamu wa Ligi Kuu ya England ‘Premier League’ umeendelea kuwa mtamu, hiyo ni baada ya kushuhudia wenyeji wa Daraja la Stamford wakiangukia pua kwa wageni wao ambao ni maarufu kwa jina la Majogoo.

Mabao mawili yaliyofungwa na Dejan Lovren na Jordan Henderson yameifanya Liverpool kupata ushindi dhidi ya Chelsea kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

Wabrazil Oscar pamoja na Coutinho wakiwa wameweka pembeni utaifa wao na wakiwania mpira kila mmoja akitaka kuinufaisha timu yake

Chelsea 1 Liverpool 2
Thibaut Courtois
Goli safi kabisa lililofungwa na nahodha wa Liverpool Jordan Henderson


Ushindi huo umeifanya Liverpool kufikisha pointi 10 na mabao 11 ya kufunga huku ikiwa imefungwa mabao nane na kulingana pointi na Chelsea na Everton iliyo katika nafasi ya pili.

Lovren aliifungia Liverpool bao la kwanza dakika ya 17 baada ya kupokea pasi ya Philippe Coutinho na bao la pili la timu hiyo lilifungwa dakika ya 36 na nahodha Henderson aliyeuwahi mpira uliookolewa na mabeki wa Chelsea.

Diego Costa
Costa akipongezana na kiuongo Matic baada ya kazi nzuri aliyoifanya na kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi
Kipindi cha pili Chelsea ilibadilika na kutawala mchezo ambao ilipata bao lake pekee dakika ya 61 kupitia kwa Diego Costa aliyepokea pasi ya Nemanja Matic. Katika mchezo huo beki wa Chelsea.

Liverpool imejiwekea rekodi nzuri katika jiji la London baada ya kujikusanyia pointi 10 ikiwa ugenini katika  jiji hilo ambapo ilianza kwa kuifunga Arsenal, kupata suluhu na Totenham na sasa kuitungua Chelsea.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA