Saturday 17 September 2016

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO MH. SAID MECK SADIKI AKABIDHI ZAWADI KWA ASKARI 34 WALIOFANYA VIZURI KATIKA UTENDAJI MWAKA 2016

 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh.Said Meck Sadiki akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Kikosi cha kutuliza ghasia FFU Moshi mjini
Sheihk kutoka ofisi ya Sheihk wa Mkoa wa Kilimanjaro akisoma dua katika sherehe hizo 

Padre kutoka ofisi ya Askofu ya  Mkoa wa Kilimanjaro akifanya maombi  katika sherehe hizo 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Wilbrod Mtafungwa akimuonesha Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh.Said Meck Sadiki baadhi ya silaha zilizokamatwa kutoka mikononi mwa wahalifu katika mkoa wa Kilimanjaro kwa mwaka 2016

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh.Said Meck Sadiki akioneshwa mihadarati aina ya bangi iliyokamatwa katika mkoa wa Kilimanjaro kwa mwaka 2016

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh.Said Meck Sadiki akikabidhi zawadi kwa baadhi ya askari waliofanya vizuri katika utendaji wao kwa mwaka 2016





Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh.Said Meck Sadiki akipokea zawadi ya piki piki mbili zenye thamani ya shilingi milioni 4  kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya  ASANTE Tours kama  sehemu ya kuunga mkono jitihada ya Jeshi hilo kuimarisha ulinzi mkoani hapa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Wilbrod Mtafungwa akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh.Said Meck Sadiki zawadi kama ishara ya ushirikiano wake katika kutimiza malengo ya kiusalama ya mkoa wa Kilimanjaro 
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh.Said Meck Sadiki  akiwahutubia wageni pamoja na wadau mbali mbali wa ulinzi na usalama mkoa wa Kilimanjaro waliofika katika sherehe hizo
Baadhi ya wadau waliohudhuria katika hafla hiyo

Na Dickson Mulashani wa Funguka Live Blog


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh Said Meck Sadiki amewatunukia zawadi askari 34 waliofanya vizuri katika tendaji wao ndani ya  jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro katika sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Kikosi cha kutuliza ghasia FFU wilaya ya Moshi mjini.
Katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na viongozi wa mkoa,wilaya pamoja na  wadau mbalimbali wa Jeshi la polisi ilianza kwa mgeni rasmi kukagua gwaride na kisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Wilbrod Mtafungwa kusoma taarifa ya ulinzi na usalama ya mkoa kuanzia mwezi Machi hadi Agusti mwaka huu.

Akiisoma taarifa hiyo mbele ya mgeni rasmi pamoja na wadua mbali mbali waliohudhuria sherehe hiyo, Kamanda Mtafungwa amesema mpaka sasa hali ni shwari na hakuna matukio yaliozua taharuki kubwa katika mkoa na akatoa takwimu za matukio kama ifuatavyo huku akizilinganisha na zile za mwaka jana. 

Mauaji -49 (Machi hadi Agusti 2015) 
              -44 (Machi hadi Agusti 2016)

Kubaka -92 (Machi hadi Agusti 2015)
               -151 (Machi hadi Agusti 2016)

Kulawiti -7 (Machi hadi Agusti 2015)
                -12 (Machi hadi Agusti 2016)

Wizi wa watoto -3 (Machi hadi Agusti 2015)
                             -4 (Machi hadi Agusti 2016)

Kusafirisha binadamu- 1 (Machi hadi Agusti 2015) 
                                                    - 0 (Machi hadi Agusti 2016)

Wizi wa kutumia silaha - 2 (Machi hadi Agusti 2015)
                                            - 1 (Machi hadi Agusti 2016)

Unyang'anyi wa kutumia silaha-29 (Machi hadi Agusti 2015)
                                                          -18 (Machi hadi Agusti 2016)

Akihutubia hadhira hiyo Mh. Said Meck Sadiki amewapongeza askari waliopata zawadi na kuwataka wasibweteke bali wajitume zaidi ili kulinda heshima waliopata leo pia amelipongeza jeshi hilo kwa ujumla kwa jitihada linazofanya ili kuendelea kudumisha utulivu mkoani hapo.

"Nawasihi muendelee kujituma na kuwatumikia wananchi kwa uadilifu mkubwa kwani wao ndio sababu ya ninyi kuwepo hivyo mkijituma katika kuwatumikia, sifa hizi zitawajengea nafasi nzuri zaidi hata ya kupanda madaraja ya vyeo lakini mkifanya tofauti lawama zao zitawafikia viongozi wenu nanyi mtawajibishwa".

Aidha Mkuu wa mkoa ambaye pia ni mwenyeketi wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa alipata nafasi ya kuoneshwa baadhi ya vitu silaha pamoja na mihadarati iliyokamatwa mikononi mwa wahalifu katika mkoa wa Kilimanjaro ambapo ni bunduki, mirungi ,bangi pamoja na madawa ya kulevya aina ya heroin.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA