Saturday 17 September 2016

MSN NI WAGAWA DOZI TU:: BARCELONA YASHINDA 5:1 DHIDI YA LEGANES

MESSI, SUAREZ NA NEYMAR WAISAMBARATISHA LEGANES KATIKA LA LIGA

Utatu mtakatifu katika soka unaoundwa na Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar umeanza kunoga tena baada ya wachezaji hao kuisaidia Barcelona kuibuka na ushindi wa magoli 5-1 dhidi ya timu ndogo ya Leganes katika ligi ya La Liga.

Katika mchezo huo Messi alikuwa wa kwanza kutikisa nyavu katika dakika ya 15 ya mchezo, na kisha Suarez kuongeza la pili katika dakika ya 31 baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Messi aliyempasia mpira.

Neymar alifunga goli la tatu katika dakika ya 44 na baadaye Messi akafunga kwa mkwaju wa penati baada ya Neymar kufanyiwa madhambi, na kisha Rafinha akafunga goli la tano, kabla ya Gabriel kuipatia Leganes goli pekee.
   Lionel Messi akifurahi baada ya kumpoteza maboya kipa wa Leganes na kuandika goli
   Luis Suarez akishangilia goli kwa kumnyooshea kidole Lionel Messi aliyempasia pasi

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA