Saturday 24 September 2016

POGBA ATOA GUNDU MAN U IKIIBUTUA LEICESTER CITY 4-1


Paul Pogba amefunga goli lake la kwanza tangu asajiliwe na Manchester United kwa ada ya paundi milioni 89, wakati Manchester United ikiwafungwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza Leicester City kwa magoli 4-1

Kikosi cha Jose Mourinho kikicheza nyumbani Old Trafford huku kapteni wake Wayne Rooney akianzia benchi kilipata goli lwa kwanza kupitia kwa kapteni wa muda Chris Smalling akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Daley Blind.

Juan Mata aliiongezea Manchester United goli la pili kabla ya Marcus Rashford hajatingisha la tatu kwa shuti la karibu na kabla ya mapumziko ndipo Paul Pogba alipofunga goli la nne kwa kichwa akiunganisha kona ya Blind, na Demarai Gray aliifungia Leicester goli pekee.
Paul Pogba akiwa ameruka juu na kupiga mpira wa kichwa ulioandika goli la nne la Manchester United 
                     Kinda hatari Marcus Rashford akiifungia Manchester United goli la tatu

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA