Tuesday 18 October 2016

DAVID DE GEA AIOKOA MAN UTD NA KUAMBULIA POINTI MOJA ANFIELD


Timu za Liverpool na Manchester United zimetoka sare tasa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza, ambao ulikuwa unafuatiliwa mno na wapenzi wa soko duniani kutokana na ushindani mkubwa ulipo baina ya timu hizo.

Katika mchezo huo shujaa alikuwa kipa wa Manchester United David de Gea, ambaye aliruka na kupangua mipira iliyopigwa na Emre Can pamoja na Philippe Coutinho kutokea umbali wa yadi 25.

Kikosi cha Jurgen Klopp kilihitaji ushindi ili kiwe na pointi sawa na vinara Manchester City, lakini kikosi cha Jose Mourinho kilicheza kwa kujilinda na kilionyesha nidhamu ya hali ya juu ya umakini.
                   Coutinho  akipiga mpira uliopanguliwa kiufundi na kipa David de Gea 
                    Kipa David de Gea akiruka kiufundi kupangua mpira uliopigwa na Coutinho
                            David de Gea tena akiokoa mpira uliopigwa na Emre Can

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA