Thursday, 27 October 2016

FARID MUSSA SASA RUKSA KUKIPIGA ULAYA


ILE sintofahamu iliyopelekea hadi nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta kuhoji kinachomkwamisha nchini Kiungo Mshambuliaji wa Azam, Farid Mussa wakati alishafuzu kucheza Ulaya, imepata jibu baada ya kibali chake cha kufanya kazi nchini Hispania kupatikana.

Farid hakujumuishwa katika kikosi cha Azam cha msimu huu baada ya kufuzu majaribio katika timu ya daraja la kwanza nchini Hispania, Club Deportivo Tenerife na sasa anaweza kuanza safari wakati wowote kwenda kuanza kuitumikia timu yake mpya.




Wiki iliyopita Samatta aliandika waraka mrefu katika ukurasa wake wa Instagram akihoji sababu za nyota huyo kuendelea kukaa nchini wakati Tenerife wakiendelea na mechi za ligi daraja la kwanza. Ujumbe huo uliwashtua wengi ndipo viongozi wa Azam walipojitokeza na kuweka wazi kuwa kinachosubiriwa ni kibali cha kufanya kazi nchini humo.

Farid anaungana na Samatta barani Ulaya huku Thomas Ulimwengu ambaye amemalizana na TP Mazembe hivi karibuni akijiandaa kutimkia zake Ulaya pia kusaka malisho mema.

Inaaminika kuwa kuongezeka kwa wachezaji wanaosakata kabumbu barani humo kutaongeza pia ubora wa kikosi cha timu ya Taifa huku hali hiyo ikifungua milango kwa makinda wengine kwenda kutafuta fursa.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA