MFUNGWA ALIYEACHIWA KWA MSAMAHA WA RAIS WIKI ILIYOPITA AKAMATWA KWA KUIBA SADAKA
Mfungwa aliyeachiwa huru kwa masamaha wa rais Uhuru Kenyatta wiki iliyopita amefikishwa mahakamani jana akikabiliwa na tuhuma za kuiba sadaka kanisani.
Mtuhumiwa huyo, Lucas Ngugi Njoroge, amefikishwa katika Mahakama ya Nyahururu mbele ya Hakimu Judith Wanjala.
Njoroge aliachiwa huru kutoka gereza la Nyahururu GK, siku ya Ijumaa baada ya rais Kenyatta kutoa msamaha kwa wafungwa siku ya Mashujaa.
Mtuhumiwa Njoroge ameshtakiwa kuwa Oktoba 23, aliiba shilingi 900 za Kenya fedha za sadaka katika Kanisa la Ol Jabet African Independent Pentecostal huko Laikipia Magharibi, kaunti Laikipia.
0 comments:
Post a Comment