Sunday 2 October 2016

SIMBA PUNGUFU YAIPOKA YANGA USHINDI DAKIKA ZA LALA SALAMA



MIAMBA ya soka nchini timu za Simba na Yanga zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 kwenye mchezo wa ligi kuu uliotawaliwa na vurugu kubwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Mechi hiyo ilianza taratibu huku timu zote zikisomana lakini dakika ya 13 Thaban Kamusoko alipata nafasi ya kuifungia Yanga bao la uongozi lakini mpira wake wa kichwa ulipaa juu ya lango kufuatia krosi ya beki Haji Mwinyi.

Amisi Tambwe aliipatia Yanga bao la kwanza dakika ya 26 baada ya mabeki wa Simba kuweka mtego wa kuotea ambapo Mrundi huyo aliwazidi akili na kumfunga golikipa Vicent Agban kirahisi.

Mwamuzi Martin Saanya kutoka mkoani Morogoro alimtoa nje nahodha wa Simba Jonas Mkude kwa kumuonesha kadi nyekundu baada ya kumzonga kutokana na kutoridhishwa na maamuzi kitu kilichopelekea vurugu na kusababisha mpira kusimama kwa dakika saba.




Licha ya kuwa pungufu Simba waliendelea kumiliki mpira ambapo kiungo Mwinyi Kazimoto aliweza kuwadhibiti Yanga hasa katika eneo la katikati ya uwanja ambapo aliweza kuvuruga mipango yote ya mabingwa hao.

Saanya aliwaonya kwa kadi ya njano Ally Mustapha, Kelvin Yondan na Mbuyu Twite wa Yanga huku Mohamed Hussein na Novaty Lufunga wakioneshwa kwa Simba.

Dakika ya 86 Shiza Kichuya aliisawazishia Simba bao baada ya kupigwa mpira wa kona ulioingia moja kwa moja wavuni na kumuacha mlinda mlango Bathez akiwa hana la kufanya.

Yanga iliwatoa Yondan, Juma Mahadhi na Deus Kaseke na kuwaingiza Andrew Vicent,Simon Msuva pamoja Haruna Niyonzima huku Simba ikiwapumzisha Ibrahim Ajib, Laudit Mavugo na Lufunga na kuwaingiza Juuko Murshid,Mohamed Ibrahim pamoja na Frederick Blagnon.

-PICHA NA BOIPLUS BLOG

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA