Saturday 22 October 2016

WAZIRI MAHIGA AFUNGUA MKUTANO WA MAJADILIANO YA AMANI NA ULINZI KATI YA SADC NA EU


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Augustine Mahiga akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye Mkutano wa majadiliano ya amani na ulinzi kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Ulaya (EU) unaofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine Mkutano huo unarajia kujadili kuhusu masuala yafuatayo; Aina za chaguzi na jinsi zinavyosimamiwa miongoni mwa nchi wanachama, Vijana wa Afrika wanaokimbilia Ulaya kutafuta maisha, tishio la amani ya Kanda  na Dunia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima (katikati) akifuatilia Mkutano. Kulia ni Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (kushoto)
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wakimsikiliza Waziri Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga
Sehemu Wajumbe wa Mkutano na Watendaji wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi kutoka SADC na EU
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akiwa katika mahojiano na wanahabari

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA