Saturday, 5 November 2016

CHELSEA YAIRARU EVERTON NA KUKWEA KILELENI LIGI KUU YA UINGEREZA

Eden Hazard amefunga magoli mawili wakati Chelsea ikitinga kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuisambaratisha Everton kwa magoli 5-0.

Hazard aliifanya Chelsea iongoze kwa kufunga goli la kwanza kwa shuti la chini, kabla ya Marcos Alonso kuongeza la pili kwa goli tobo lililopita miguuni mwa Maarten Stekelenburg.

Diego Costa aliongeza goli la tatu kabla ya mapumziko na kisha Hazard kufunga tena kufumania nyavu, ambapo Pedro alikamilisha karamu hiyo ya magoli kwa kufunga goli la tano.
       Eden Hazrad akijipinda na kuachia shuti ambalo lilijaa wavuni na kuandika goli 
                 Diego Costa akishangilia goli baada ya kumpoteza golikipa maboyo na kufunga 
               Kocha wa Chelsea Antonio Conte akishangilia goli pamoja na wachezaji wake 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA