Saturday 19 November 2016

GIROUD AIKOMBOA ARSENAL NA KULAZIMISHA SARE NA MANCHESTER UNITED DAKIKA ZA MWISHO



Goli la kusawazisha la Olivier Giroud la dakika ya 89, limeipatia Arsenal pointi moja na kuinyima Manchester United ushindi ambao walikuwa wakishahili kuupata katika dimba la Old Trafford.

Katika mchezo huo Juan Mata aliifungia Manchester United goli la kwanza kwa shuti la guu la kushoto, akiunganisha pasi ya Ander Herrera katika dakika ya 68.

Arsenal walikuwa hawajafanya jitihada zozote makini za kutafuta goli walijikuta wakisawazisha goli hilo kupiti Giroud aliyeunganishwa kwa kichwa krosi ya Alex Oxlade-Chamberlain.

          Kipa Petr Cech akiwa hana la kufanya baada ya kushindwa kuzuia shuti la Juan Mata
  Mshambuliaji Oliver Giroud akiwa ameruka juu na kupiga mpira kwa kichwa uliosawazisha goli

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA