Tuesday, 15 November 2016

MWIGULU AFANYA ZIARA MAKAO MAKUU UHAMIAJI, ATEMBELEA NYUMBA ZA MAKAMISHNA NA KIWANDA CHA UCHAPISHAJI NYARAKA


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (aliyevaa tai) akikaribishwa na Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Victoria Lembeli (kulia) pamoja na maafisa waandamizi wa Idara hiyo katika ofisi za Makao Makuu, Kurasini jijini Dar es Salaam. Mwigulu alifanya ziara katika idara hiyo kwa kutembelea maeneo ya utendaji katika ofisi hizo, alizungumza na maafisa na askari Uhamiaji na baadaye alitembelea mradi wa nyumba za Makamishna na Kiwanda cha Uchapishaji Nyaraka za Uhamiaji, zilizopo Kijichi jijini humo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia) akizungumza na wateja waliofika kupata huduma katika ofisi za Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli Mwigulu alifanya ziara katika idara hiyo kwa kutembelea maeneo ya utendaji katika ofisi hizo, alizungumza na maafisa na askari Uhamiaji na baadaye alitembelea mradi wa nyumba za Makamishna na Kiwanda cha Uchapishaji Nyaraka za Uhamiaji, zilizopo Kijichi jijini humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na Makamishna, Maafisa na Askari wa Uhamiaji katika ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam. Mwigulu aliwaambia aliwapongeza watumishi hao kwa kazi nzuri wanayoifanya na aliwataka waongeze juhudi zaidi ya kuwakamata wahamiaji haramu na kuwachukulia hatua kali bila kuwaonea watu katika ukamataji wao. Waziri huyo alifanya ziara katika idara hiyo kwa kutembelea maeneo ya utendaji katika ofisi hizo na baadaye alitembelea mradi wa nyumba za Makamishna na Kiwanda cha Uchapishaji Nyaraka za Uhamiaji, zilizopo Kijichi jijini humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsikiliza Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli (kulia) alipokuwa anatoa hotuba fupi na baadaye kumkaribisha Waziri huyo kuzungumza na maafisa na askari wa Uhamiaji wa Makao Makuu wa Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake Waziri Mwigulu aliwataka askari hao waongeze juhudi zaidi ya kuwakamata wahamiaji haramu na kuwachukulia hatua kali bila kuwaonea watu katika ukamataji wao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (aliyevaa tai) na Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli wakitoka moja ya nyumba zinazojengwa kwa ajili ya Makamishna wa Uhamiaji, Kijichi, jijini Dar es Salaam. Waziri Mwigulu alizikagua nyumba hizo ambazo zipo hatua za mwisho kukamilika. Waziri huyo alifanya ziara katika idara hiyo kwa kutembelea maeneo ya utendaji katika ofisi hizo na baadaye alitembelea mradi wa nyumba za Makamishna na Kiwanda cha Uchapishaji Nyaraka za Uhamiaji, zilizopo Kijichi jijini humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (aliyevaa tai) akiangalia fomu za kuomba pasipoti za Idara ya Uhamiaji mara baada ya kuchapishwa katika kiwanda hicho kilichopo Kijichi, jijini Dar es Salaam. Waziri Mwigulu alikitembelea kiwanda hicho pamoja na Mradi wa nyumba za Makamishna zinazojengwa katika eneo hilo. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA