Sunday 20 November 2016

PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG AIBEBA DORTMUND DHIDI YA BAYERN MUNICH

Goli la kipindi cha kwanza la Pierre-Emerick Aubameyang, limeipatia Borussia Dortmund ushindi dhidi ya Bayern Munich katika mchezo huo wa miamba ya Ujerumani.

Aubameyang aliunganisha krosi ya chini ya Mario Gotze iliyompita kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer, na kuifanya Dortmund kuongoza katika dakika ya 11 ya mchezo huo.

Katika mchezo huo Frank Ribery alifunga goli kwa kisigino katika kipindi cha pili lakini kibendera kilinyooshwa juu kuashiria kuwa ameotea.
                           Pierre-Emerick Aubameyang akifunga goli pekee katika mchezo huo
          Franck Ribery akifunga goli kwa kisigino ambalo lilikataliwa kutokana na kuotea 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA