TANZIA: MBUNGE WA DIMANI, HAFIDH ALLY TAHIR AFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA LEO DODOMA
Hafidh Ally Tahir (enzi za uhai wake) |
Mhe Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tannzaia anasikitika kuwatangazia kuwa aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar Mheshimiwa Hafidh Ali Tahir amefariki dunia asubuhi ya kuamkia leo katika Hospitali ya General mkoani Dodoma.
Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitatolewa hapo baadae. Mhe Spika anaungana na Wabunge wote katika kuomboleza msiba huu.
Awali Marehemu pia alikuwa mwalimu wa soka kwenye timu ya Bunge Sports Club na mpaka usiku wa Novemba 10 alikuwa pamoja na waheshimiwa wabunge katika vikao.
0 comments:
Post a Comment