Showing posts with label BUNGE. Show all posts
Showing posts with label BUNGE. Show all posts

Wednesday, 3 November 2021

MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA 2022-2023 YAWASILISHWA BUNGENI

 

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwasilisha bungeni Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2022/23, jijini Dodoma.




Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akifurahia jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), baada ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2022/23, bungeni, jijini Dodoma.



Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoa wa Lindi, Mhe. Moses Nnauye, kabla ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2022/23, bungeni, jijini Dodoma.



Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wa pili kushoto, Kamishna wa Bajeti wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Balandya Elikana (kulia), akiwa na viongozi wengine, baada ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2022/23, bungeni Dodoma.


Kamishna wa Bajeti wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Balandya Elikana (kushoto), Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera wa Wizara hiyo Bw. Mbayan Saruni, wakiwa na viongozi wengine wa Wizara hiyo katika viwanja vya Bunge, jijini Dodoma, baada ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2022/23.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango)


Tuesday, 26 September 2017

ZUNGU: BUNGE HALITATUNGA SHERIA YA KUZUIA MIMBA SHULENI, HILO NI JUKUMU LA WAZAZI

Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu amesema hakuna sheria itakayotungwa na chombo hicho itakayozuia mimba shuleni na kuwataka wazazi kuwajibika kutoa malezi bora kwa watoto wao ili wasipate ujauzito.

Zungu aliyasema hayo jana kwenye mahafali ya 15 ya kidato cha nne katika Sekondari ya Wasichana ya Barbro Johansson akimwakilisha Spika Job Ndugai.

Alisema jukumu la kudhibiti mimba halipaswi kutegemee sheria pekee na kwamba, wazazi wanawajibika kuhakikisha wanatoa malezi bora kwa kuwa baadhi ya tabia zao zinaendana na watoto wao.

“Ukiona mtoto ni mhuni ujue na mzazi wake ni mhuni, mtoto akiwa na nidhamu na mzazi wake ana nidhamu,” alisema Zungu na kuibua gumzo miongoni mwa wazazi waliofika shuleni hapo.

“Ni jukumu la wazazi kuwalea vizuri watoto wenu na kuhakikisha hawajiingizi katika makundi hatarishi.”

Zungu ambaye pia ni mbunge wa Ilala aliwataka wanafunzi kutojihusisha na masuala ya kisiasa shuleni, bali wajikite katika masomo kwa manufaa yao.

“Kilimo ni njia ya kujikwamua kiuchumi, lakini najua vijana wengi hampendi kilimo. Niwaambieni jishughulisheni na kilimo kama sehemu ya ajira,” aliwaambia wahitimu 116 watakaohitimu.

Mbunge wa Muleba Kusini, Anna Tibaijuka alisema ni lazima jamii ikubaliane na agizo la Rais John Magufuli la kuwataka wanafunzi wanaopata mimba kutoendelea na masomo.

Tibaijuka ambaye pia ni mwenyekiti mwanzilishi wa taasisi hiyo, alisema kuwaruhusu wanafunzi wanaopata mimba kuendelea na masomo ni kuongeza tatizo .

Mkuu wa shule hiyo, Halima Kamote alisema licha ya kuwa na wanafunzi wa kike zaidi ya 600, hakuna aliyepata mimba akiwa shuleni kutokana na malezi mazuri kwa kushirikiana na wazazi.

Sunday, 24 September 2017

BUNGE LAWEKA WAZI NYARAKA KUHUSU KUWASLISHA MCHANGO WA MATIBABU YA TUNDU LISSU


Sunday, September 24, 2017

Bunge Laijibu Hospitali ya Kenya Anakotibiwa Tundu Lissu

Seebait.com 2017SeeBait
Ofisi ya Bunge imetoa uthibitisho wa nyaraka kuonyesha kuwa fedha zilizochangwa na wabunge zimewasilishwa hospitalini anakotibiwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Lissu aliyeshambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma Septemba 7, anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

“Napenda kusisitiza kuwa fedha zilizochangwa na wabunge Sh43 milioni kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Mheshimiwa Tundu Lissu tayari zimetumwa katika Akaunti ya Hospitali ya Nairobi anakopatiwa matibabu,” imesema taarifa iliyotolewa leo Jumapili na Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mawasiliano cha Bunge.

Fedha hizo zimetumwa kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Bunge limesema fedha hizo ambapo kwa mujibu wa viwango vya kubadilishia fedha vya BoT kwa siku hiyo ili kuwa ni sawa na Shilingi ya Kenya 1,977,120.58.

“Kiasi hicho cha Fedha kilitumwa Septemba 20, 2017 kwenda Benki ya Barclays, Tawi la Hurlringham, Akaunti Namba 0451155318 yenye jina la Kenya Hospital Association.

Thursday, 27 July 2017

BUNGE LARIDHIA KUVULIWA UANACHAMA WABUNGE 8 WA CUF

Image result for bunge la tanzania 2017
Siku moja baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kupokea barua kutoka kwa Mwenyekiti wa CUF Taifa anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili, Prof. Ibrahim Lipumba inayoeleza kuwafukuza uanachama Wabunge wanane wa Viti Maalum na Madiwani wawili, Bunge limeridhia.

Leo July 26, 2017 taarifa kutoka ofisi ya Bunge imeeleza kuwa Spika Job Ndugai ameridhia kufutwa uanachama kwa Wabunge hao na hivyo nafasi zao ziko wazi.

Monday, 26 June 2017

SPIKA NDUGAI:: LICHA YA TOFAUTI ZETU WABUNGE TUNAPASWA KUSHIRIKIANA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Job Ndugai amewakumbusha wabunge wa vyama vya upinzani hasa vinavyounda UKAWA umuhimu wa jamii kukaa pamoja, kujadiliana na kumaliza tofauti zao.

Ndugai ambaye ni mmoja wa wabunge wa Bunge la 11 aliyasema hayo baada ya baadhi ya wabunge hasa wa upinzani kususia futari aliyoiandaa siku ya Jumanne kwa ajili ya wabunge wote. Kiongozi huyo wa juu wa mhimili huo alisema kuwa licha ya jukumu zito la kujadili na kupitish bajeti ya serikali ya 2017/2018, ushirikiano kwa jamii ni muhimu.

Jambo hilo lilmfanya asiwe na raha na kuamua kuzungumzia ndani ya bunge kwa upole kabisa ambapo alisema kuwa, baada ya kuhudhuria futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Jumatatu, na baada ya kuwepo tetesi za kususia ya kwake alisema, amejifunza kuwa baadhi wamekatazana kuhudhuria shughuli kama hizo.

“Lakini nikajifunza kitu kimoja ambacho sikupenda kukisema, ila nikiseme hapa kidogo. Kuna wenzetu wamekatazana rasmi kuhudhuria shughuli kama hizi.”

Ndugai aliyasema hayo Jumanne wakati akihitimisha kipindi cha maswali na majibu kabla ya kupisha mapumziko na kisha kupigiwa kura kwa bajeti ya serikali.

"Bunge linaendeshwa kwa mawasiliano ya namna mbalimbali baina ya wabunge na uongozi.  Endapo kuna jambo linakwaza na kusababisha watu wasipate futari pamoja,  ni vizuri wakae pamoja na kuondoa jambo hilo," alizungumza Ndugai.

Licha ya kutoa tahadhari hiyo, Ndugai alisema kuwa wabunge hao wana uhuru wa kufanya hivyo (kutohudhuria) kama wanaona ni sawasawa.

“Siyo mwezi wa chuki na kubaguana. Niwakaribishe tena kwenye futari kwa watakaoweza kufika. Watakaoshindwa In Sha Allah, kila la heri. Tutaendelea kuwa pamoja mjengo huu huu,” alisema Spika Ndugai akihitimisha nasaha zake.

Monday, 5 June 2017

MBUNGE KESSY ASHAURI WALIOSAINI MIKATABA MIBOVU YA MADINI WANYONGWE

Mbunge wa Nkasi (CCM), Ally Kessy amefunguka na kusema watu waliohusika kusaini mikataba mibovu ya madini wanatakiwa kunyongwa kwani nchi ikitapoteza watu ishirini au thelathini hakuna hasara yoyote.

Mbunge Kessy anasema kama watu hao waliotia saini ya mikataba ya madini mwaka 1998 watakamatwa na mali zao kunyang'anywa na wakanyongwa itakuwa ni fundisho kubwa kwa watu wengine na baadhi ya wabunge wengine waliunga mkono hoja hiyo huku wakitaka mikataba hiyo ya madini iweze kupitiwa upya.

"Wakamatwe wote waliohusika na mikataba mibovu na kusababisha kuingizia serikali hasara, ikiwezekana wanyongwe hata ishirini au thelathini maana nchi hii wanazaliwa watu Muhimbili zaidi ya mia moja kwa siku, Bungando wanazaliwa mpaka Namanyele wanazaliwa kwa hiyo tukipoteza watu mia moja au mia mbili Mh. Spika hakuna kitu kitakachopotea katika nchi hii, tumeonewa vya kutosha haiwezekani"alisisitiza Ally Kessy na kuongeza;

"Mnasema mnarekebisha mikataba, mikataba kurekebisha ni kutafuta hao wote waliosaini wakamatwe, wanyang'anywe mali zao, wanyongwe tutabaki salama katika hii nchi, itakuwa mfano, nataka comment ya serikali kusikia kuwa tutashughulikia wote waliotia saini mikataba ya madini 1998 wakamatwe mara moja" alisema Kessy

Tuesday, 21 March 2017

MWENYEKITI NA MAKAMU WAKE , KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA NA BIASHARA WAJIUZULU NYADHIFA ZAO

Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara Dk Dalali Kafumu na makamu wa kamati hiyo Vick Kamata, kwa pamoja wamejiuzulu nafasi zao.

Viongozi hao wameeleza sababu za kuchukua hatua hiyo kuwa ni serikali kuingilia majukumu yao katika utendaji kazi na hivyo wakaeleza kuwa hawaoni sababu za kuendelea na majukumu hayo.

Wamekabidhi barua za kujiuzulu kwenye ofisi ya spika wa bunge jana.

Thursday, 19 January 2017

EALA HAILS RWANDA AS IT MULLS OVER INTRODUCING KISWAHILI AS ONE OF THE OFFICIAL LANGUAGES

Hon Shyrose Bhanji, the mover of the Resolution justifies the Motion 
 Hon Nancy Abisai who rose in support of the Resolution congratulating Rwanda for its initiatives to introduce Kiswahili as an official language
Minister for State, EAC Affairs, Republic of Uganda, Hon Wandera Julius Maganda on the floor of the House

EALA this morning congratulated Government of Rwanda following its move to start a legislative process towards making Kiswahili one of the official languages in the country.

The Resolution passed this morning and moved by Hon Shyrose Bhanji, follows a Cabinet Meeting held on October 12th, 2016 in Rwanda, that passed the draft law seeking to make Kiswahili one of the official languages of the Assembly.  

The move now awaits the consideration, discussion and approval by the Parliament of Rwanda before becoming law. The Assembly thus urges Parliament of Rwanda to expeditiously consider the Cabinet’s Resolution

Article 119 of the EAC Treaty, provides for the development and promotion of indigenous languages especially Kiswahili as a lingua franca of the region.

Kiswahili is not only a unifying language spoken by East Africans but it is rich in dialect and expression. 

“It is widely spoken in the EAC countries as well as some countries in the Central and Southern part of Africa making it one of the most popular language spoken in the Continent after Arabic”, the Resolution says in part.

Justifying the Motion, Hon Shyrose Bhanji hailed the President of Rwanda, H.E. Paul Kagame and the Cabinet for the decision to begin the process of making Kiswahili an official language. She urged the citizens of the country to embrace Kiswahili, which she termed the language of unity.

At debate time, Hon Martin Ngoga said Kiswahili was a strong unifying tool and that it would make the integration story to be less elitist. “Definitely, Kiswahili will create a strong bond among East Africans”, Hon Ngoga said.   “I congratulate the mover”, he added.


Hon Nancy Abisai remarked that sensitization about the Kiswahili language was key especially in Uganda to enhance awareness amongst the citizens given that Kiswahili is a common language for the region.

Hon Abubakar Zein said the region was waiting and looking forward to the time when the Assembly would embrace Kiswahili in its debates.  “All Heads of State in the Community have embraced Kiswahili.  It is a beautiful language”, he said.

On his part, Hon Adam Kimbisa said the citizens of East African Community were the custodians of Swahili and need to guide and guard the language.  “Rwanda has thus shown the way in the process of east africanisation of the language”, he added.

Hon Joseph Kiangoi however remarked that it was important for the Cabinet Resolution to be brought to the House (EALA) to inform the regional Assembly. Hon AbuBakr Ogle said there were pertinent issues to be considered once Kiswahili becomes an official language including translation of vital documents.

Others who contributed to the debate were Hon Mike Sebalu, Hon Patricia Hajabakiga, Hon Dora Byamukama and the Minister for State for EAC Affairs, Hon Wandera Julius Maganda.

In August 2016, EALA passed a Resolution to urge the Summit of EAC to amend the Treaty for the establishment of the Community to provide for Kiswahili as one of the official Languages of the Community.

At the same time, the Assembly urged the Council of Ministers to allocate adequate resources to EAC Kiswahili Commission to effectively carry out its mandate.

Saturday, 12 November 2016

PICHA::WAZIRI MKUU AONGOZA WABUNGE KUAGA MWILI WA SITTA BUNGENI,


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Spika Mstaafu, Samuel Sitta, bungeni mjini Dodoma, Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)​
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye jeneza la Spika Mstaafu Samwel Sitta, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Mstaafu, Samuel Malecela akimpa pole mjane wa Spika Mstaafu, Margareth Sitta bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa (wapili kulia) akimfariji mjane wa Spika Mstaafu Mama Margareth Sitta baada ya mwili wa Spika Mstaafu, Marehemu Samuel Sita kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao maalum cha bunge cha kumuenzi Spika Mstaafu, Samuel Sitta, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Mwili wa Spika Mstaafu, Samuel Sitta ukiingizwa bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)


Mwili wa Spika Mstaafu Samuel Sitta ukiteremshwa kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai pamoja na viongozi wengine wakiusubiri mwili wa Spika mstaafu, Samuel Sitta uteremshwe kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Friday, 11 November 2016

TANZIA: MBUNGE WA DIMANI, HAFIDH ALLY TAHIR AFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA LEO DODOMA


Mbunge wa Dimani Tahiri Ally
Hafidh Ally Tahir  (enzi za uhai wake)

Mhe Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tannzaia  anasikitika kuwatangazia kuwa aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar Mheshimiwa Hafidh Ali Tahir amefariki dunia asubuhi ya kuamkia leo katika Hospitali ya General mkoani Dodoma.
Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitatolewa hapo baadae. Mhe Spika anaungana na Wabunge wote katika kuomboleza msiba huu.
Awali Marehemu pia alikuwa mwalimu wa soka kwenye timu ya Bunge Sports Club na mpaka usiku wa Novemba 10 alikuwa pamoja na waheshimiwa wabunge katika vikao.

Monday, 7 November 2016

MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA

Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azan Zugu akiongozwa na Mpambe wa Bunge kutoka baada ya kuahirisha kikao cha Bunge ili kuomboleza Kifo cha Spika Mstaafu, Samuel Sitta, mjini Dodoma Novemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mwenyekiti wa Bunge , Mussa Azzan Zungu akiahirisha kikao cha Bunge ili kuomboleza Kifo cha Spika Mstaafu, Samuel Sitta, mjini Dodoma Novemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanakwaya wa Kwaya ya Zaburi kutoka Usharika wa Ulemo KKKT Iramba kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Novemba 7, 2016. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Wabunge wakizungumza baada ya bunge kuahirishwa mjini Dodoma Novemba 7, 2016 kufuatia kifo cha Spika Mstaafu,Samuel Sitta. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, Mbunge wa Viti Malum Felista Bura, Mbunge wa Viti Maalum, Shally Josepha Raymond, Mbunge wa Musoma Mjini Mathayo Manyinyi, Mbunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe, Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Tekinolojia, Mhandisi Stella Manyanya na Mbunge wa Busanda, Lolesia `Bukwimba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju akiteta na Mwanansheria Mkuu wa Serikali Mstaafu na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (kulia) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mwenyekiti wa Bunge , Mussa Azzan Zungu akiahirisha kikao cha Bunge ili kuomboleza Kifo cha Spika Mstaafu, Samuel Sitta, mjini Dodoma Novemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanakwaya wa Kwaya ya Zaburi kutoka Usharika wa Ulemo KKKT Iramba kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Novemba 7, 2016. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanakwaya wa Kwaya ya Zaburi kutoka Usharika wa Ulemo KKKT Iramba kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Novemba 7, 2016. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanakwaya wa Kwaya ya Zaburi kutoka Usharika wa Ulemo KKKT Iramba kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Novemba 7, 2016. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanakwaya wa Kwaya ya Zaburi kutoka Usharika wa Ulemo KKKT Iramba kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Novemba 7, 2016. Kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Mary Mwanjelwa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju akiteta na Mwanansheria Mkuu wa Serikali Mstaafu na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (kulia) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju akiteta na Mwanansheria Mkuu wa Serikali Mstaafu na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (kulia) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA