Friday 11 November 2016

USHINDI DHIDI YA RUVU SHOOTING WAISOGEZA YANGA KUIPUMULIA SIMBA

YANGA imepunguza idadi ya pointi hadi kufikia mbili nyuma ya vinara Simba baada ya kuwafunga Maafande wa Ruvu Shooting mabao 2-1 katika mchezo wa kumalizia duru la kwanza la ligi kuu ya Vodacom uliopigwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mzunguko wa kwanza wa ligi umemalizika  huku Mabingwa hao watetezi wakimaliza nafasi ya pili baada ya kujikusanyia alama 33 katika michezo 15 iliyoshuka dimbani.

Abraham Mussa alikuwa wa kwanza kuwapatia Ruvu bao dakika ya 7 baada ya kupokea pasi ya Saidi Madega kabla ya kuichambua safu ya ulinzi wa Yanga na kumfunga kirahisi mlinda mlango Beno Kakolanya.


Simon Msuva alisawazisha bao hilo dakika ya 32 baada ya kupokea pasi iliyopigwa kiufundi na Haruna Niyonzima kutokana na safu ya ulinzi ya Ruvu kuzembea kuondoa hatari langoni mwao.

Kocha wa Yanga Hans Pluijm alitolewa uwanjani baada kuzozana na mwamuzi Mathew Akrama kutoka jijini Mwanza mwishoni mwa kipindi cha kwanza kutokana na kutoridhishwa na maamuzi yake.

Niyonzima aliipatia Yanga bao la pili dakika ya 59 baada ya kupokea mpira kutoka kwa Donald Ngoma aliyefanya jitihada binafsi kabla ya kutoa pasi ya mwisho kwa nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Rwanda.


Yanga iliwatoa Obrey Chirwa na Ngoma na kuwaingiza Juma Mahadhi pamoja na Matheo Anthony huku Ruvu wakiwapumzisha Fully Maganga na Mau Bofu nafasi zao zikachukuliwa na Saidi Dilunga na Yusuph Nguya.
credit BOIPLUS Blog

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA