Cristiano Ronaldo amefunga magoli matatu 'hat trick' na kuisaidia Real Madrid kutwaa kombe la klabu bingwa dunia kwa ushindi wa magoli 4-2 dhidi ya Kashima Antlers.
Ronaldo alifunga goli moja kwa mkwaju wa penati na kisha kutupia mengine mawili katika dakika za nyongeza za michezo.
Karim Benzema alikuwa wa kwanza kufunga goli katika mchezo huo, lakini Gaku Shibasaki akaisawazishia Kashima, na kisha katika kipindi cha pili Shibashaki akafunga la pili.
Cristiano Ronaldo akifunga goli kwa shuti la penati
Gaku Shibasaki akiifungia Kshima goli katika mchezo huo wa fainali
0 comments:
Post a Comment