Monday, 19 December 2016

LUIS SUAREZ ATUPIA MAWILI , BARCELONA IKIJIKITA NAFASI YA PILI LA LIGA

Luis Suarez ametupia magoli mawili wakati Barcelona ikikwea hadi katika nafasi ya pili ya msimamo wa La Liga baada ya kupata ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Espanyol.

Suarez alifunga goli la kwanza kwa kutoka kasi na kumalizia kiurahisi, kabla ya kufunga la pili kwa shuti la karibu na goli.

Jordi Alba aliifungia Barcelona goli la tatu, na David Lopez akaifungia Espanyol goli pekee kabla ya Lionel Messi kufunga la nne.
                              Luis Suarez akiwa ameupiga mpira uliomshinda kipa Diego Lopez 
                                       Mbrazil Neymar akionyesha maujuzi yake ya kupiga chenga

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA