Tuesday, 27 December 2016

LIGI KUU UINGEREZA::CHELSEA YAJIWEKA ALAMA TISA ZAIDI KILELENI

Chelsea 3-0 Bournemouth: Eden Hazard scores his 50th Premier League goal
Timu ya Chelsea inaongoza Kigi Kuu ya Uingereza kwa tofauti ya pointi 9 ikijikita kileleni baada ya kuifunga Bournemouth magoli 3-0 na kuweka rekodi ya kushinda michezo 12 mfululizo ya ligi hiyo.

Cesc Fabregas alimtengenezea goli Pedro aliyetikisa nyavu kwa shuti la mpira uliobadili muelekeo na kutinga kwenye kona ya juu ya goli, huku Eden Hazrad akifunga goli la pili kwa mkwaju wa penati baada ya kuangushwa na Simon Francis.

Pedro aliongeza goli la tatu katika muda wa majeruhi baada mpira walioupiga kwa shuti kali kumgonga Steve Cook na mpira kukatiza kwenye mstari wa goli.
                                          Mchezaji wa Chelsea Pedro akiachia shuti lililozaa goli
                Eden Hazard akikwatuliwa na Simon Francis na kupatatiwa penati

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA