Thursday 19 January 2017

MTIBWA WAIPUNGUZA SIMBA MAKALI YA KUWANIA UBINGWA


Image result for SIMBA VS MTIBWA
Akram Msangi, Morogoro
SARE tasa waliyopata wekundu wa Msimbazi Simba jioni hii dhidi ya Mtibwa Sugar katika dimba la Jamhuri Morogoro imeongeza pointi moja zaidi na kufanya tofauti kati yao na Yanga kuwa pointi mbili.

Hapo jana mabingwa hao watetezi wa ligi kuu waliipiga Majimaji bao 1-0 na kupunguza 'shimo' kati yao na Simba ambalo lilikuwa alama nne na kubakisha moja, lakini kwa sare ya leo Simba wamepiga hatua moja zaidi.

Mchezo kati ya Simba na Mtibwa ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka nchini hasa baada ya Simba kushindwa kutwaa kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 toka kwa Azam FC hivyo ikiaminika gadhabu zao zingewaangukia vijana hao wa Manungu.




Katika mchezo huo mgumu na wa kasi ulishuhudiwa timu hizo zikishambuliana kwa zamu lakini umakini mdogo wa washambuliaji uliwanyima raha ya mechi watazamaji ambao waliondoka uwanjani bila kushuhudia bao lolote.

Mabadili ya wachezaji kwa timu zote hayakuweza kubadili upepo Simba ikiwatoa Shiza Kichuya, Mwinyi Kazimoto na Laudit Mavugo nafasi zao zikichukuliwa na Jamali Mnyate, Pastory Athanas na Ibrahim Ajibu huku Mtibwa wao wakiwatoa Jaffar Salum na Vicent Barnabas na kuwaingiza Hussein Javu na Kelvin Friday.

Matokeo hayo yameipeleka Mtibwa hadi nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 31 nyuma ya Simba (45) na Yanga (43)

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA