Wednesday, 11 January 2017

SIMBA YAITAMBIA YANGA NA KUSONGA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI

Image result for kikosi cha simba mapinduzi cup 2017
PICHA TOKA MAKTABA
Yanga ilijikuta ikiendelea kusulubiwa kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup baada ya kujikuta ikichezea kichapo kutoka kwa Simba kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili kwa mikwaju ya penati 4-2 kufatia dakika 90 kumalizika bila timu hizo kufungana.

Baada kichapo cha 4-0 kutoka kwa Azam FC, Yanga imeondoshwa kwenye michuano hiyo na kuziacha Simba na Azam zikutane kwenye mchezo wa fainali ambao utachezwa siku ya Ijumaa January 13, 2017 ikiwa ni siku moja baada ya kilele cha Mapinduzi ya Zanzibar.

Golikipa wa Simba Daniel Agyei ndio alikuwa shujaa kwa upande wa Simba hususan kwenye changamoto ya mikwaju ya penati. Agyei ameokoa penati mbili za Deogratius Munishi na Mwinyi Haji huku yeye akifunga penati yake baada ya Mkude kufunga ya kwanza.

Wachezaji wa Simba waliofunga penati: Jonas Mkude, Daniel Agyei, Mzamiru Yassin na Javier Boukungu

Method Manjale ni mchezaji pekee wa Simba aliyekosa penati ambayo iliokolewa na golikipa wa Yanga Deogratius Munishi.

Simon Msuva na Thaban Kamusoko ndio wachezaji pekee wa Yanga waliofunga penati zao huku Deogratius Minish ‘Dida’ na Mwinyi Haji penati zao zilitua kwenye mikono ya golikipa wa Simba Daniel Agyei.

Mchezo huo ulianza kwa kasi kiasi ambapo timu zote zilishambuliana kwa zamu huku zikicheza kwa tahadhari kubwa kuhakikisha nyavu zao hazitikiswi na mpira ukichezwa zaidi eneo la katikati ya uwanja.

Kiungo Mohammed Ibrahim wa Simba alipata nafasi ya kufunga dakika ya 43 na shuti lake la mguu wa kushoto likagonga mwamba huku Juma Liuzio akishindwa kumalizia baada ya mpira kumfuata mguuni.

Kocha wa Simba Joseph Omog ambaye muda mwingi wa mchezo alikuwa amesimama kutoa maelekezo kwa wachezaji wake aliwatoa Shiza Kichuya,Liuzio na Ibrahim nafasi zao zikachuliwa na Jamal Mnyate, Pastory Athanas pamoja Laudit Mavugo huku Yanga ikimuingiza Emmanuel Martin kuchukua nafasi ya Deus Kaseke.

Huu unakuwa mchezo wa tano baina ya timu hizo kukutana kwenye uwanja huo ambapo Simba wameshinda mechi nne na Yanga wakiibuka na ushindi mara moja.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA