Saturday 11 March 2017

UN: DUNIA YAKABILIWA NA JANGA KUBWA LA BAA LA NJAA

Image result for HUNGER CRISIS
Picha na Mtandao
Dunia inakabiliwa na janga kubwa la kibinadamu kuwahi kutokea tangu mwaka 1945, Umoja wa Mataifa umesema na kutoa ombi kusaidia kuepusha janga hilo.

Mkuu wa Misaada ya Kibinadamu Stephen O'Brien amesema zaidi ya watu milioni 20 wanakabiliwa na tishio la njaa na ukame katika mataifa ya Yemen, Somalia, Sudani Kusini na Nigeria.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto (Unicef) limeshaonya kuwa watoto milioni 1.4 watakufa njaa mwaka huu.

Bw. O'Brien amesema kuwa dola bilioni 4.4 za Marekani zinahitajika ifikapo Julai mwaka huu ili kuepuka janga la baa la njaa.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA