MUFTI WA TANZANIA AWAASA WASILAMU NCHINI KUITUNZA AMANI
SHEIKH Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakary Bin Zubeiry, amewaasa Waislamu nchini kuitunza amani kwani ni kama yai.
"Unajua yai lilivyo, ukilichezea likakuponyoka na kudondoka chini, huwezi tena kulikusanya na kulitumia, hivyo niwajibu wetu sisi Waislamu na wananchi kwa ujumla kuitunza amani tuliyo nayo na huu ndio ujumbe wangu muhimu kwa leo hii." Alifafanua Mufti Zubeiry baada ya ibada ya sala ya Eid Al Edh'ha na Baraza la Eid lililofanyika Masjid (Msikiti) wa Taqwa, ulioko Ilala Bungoni jijini Dar es Salaam leo asubuhi Septemba 1, 2017.
Mufti Zubeiry amesema, Mwenyezimungu aliwaambia waliofarakana kuwa hawawezi kuingia peponi mpaka wakapatane kwanza, na kwa hakika tunawaomba watu wote waliohitilafiana, wenye chuki, wenye vinyongo, wenye vifundo, waondoshe na leo ndio siku ya kukaa pamoja na kula pamoja, katika sikukuu hii ya Eid al hadh'ha, alisema Mufti.
0 comments:
Post a Comment