Tuesday, 14 November 2017

SHIRIKA LA AMREF LAZINDUA MRADI WA UCHECHEMUZI KATIKA SEKTA YA AFYA MKOANI SHINYANGA

Shirika la Amref Health Africa hii leo limezindua mradi wa uchechemuzi katika sekta ya afya (Health System Advocacy HSA) mkoani Shinyanga, wenye lengo la kuongeza ushawishi katika sekta ya afya ili kuboresha zaidi sekta hiyo mkoani humo. Meneja mradi huo, Josiah Otege amesema lengo ni kufanya uchechemuzi (ushawishi) katika maeneo manne ya sekta ya afya ambayo ni kuimarisha uzazi wa upango, bajeti ya afya, kuongeza idadi ya watumishi wa afya, kuboresha afya ya uzazi pamoja na utawala bora katika sekta hiyo. 

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, mgeni rasmi Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dkt.Rashid Mfaume ambaye alimwakilisha Katibu Tawala mkoani humo Albert Msovela, alilipongeza shirika la Amref kwa kuanzisha mradi huo ambao alisema utasimamiwa vyema ili kuhakikisha unaleta mabadiliko chanya katika jamii. Mradi huo ambao ni wa miaka minne kuanzia mwaka huu, unatarajiwa kutekelezwa katika halmashauri tatu za mkoa wa shinyanga ambazo ni Msalala, Shinyanga Vijijini pamoja na Kishapu.

  Meneja mradi huo wa HSA, Josiah Otege akizungumzia mradi huo.


 

Na Binagi Media Group

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA