MBINU SITA (6) SAHIHI ZA KUWEKA AKIBA ZAIDI NA KUWEKEZA VIZURI.
Kuna mambo
mengi unayotaka kuyafanikisha katika kipindi hiki cha maisha yako. Bila ya
kukanusha ,Ukweli ni kwamba baadhi ya ndoto zako zina gharimu fedha. Na ufunguo
wa kuzifanikisha ndoto hizo ni kujifunza kusimamia fedha.
Pale
unapokuwa umeshajifunza misingi ya kuhifadhi au kuweka akiba na kuwekeza fedha,
bila shaka utaweza kuyafanikisha malengo yako.
Katika
uchumi wa sasa wenye uhaba wa nishati na gharama za vyakula kuwa kubwa na kukua
kwa kasi ya ukosefu wa ajira, kusimamia fedha kunaweza kukawa ni kazi ngumu
sana ,lakini kwa hakika hakuna hata jambo moja lisilowezekana .Unawezaje kwenda
na hali hii? Zifuatazo ni mbinu sita za kuweza kuweka akiba fedha nyingi zaidi
na kuwekeza vizuri.
1. kuweka bajeti ni kipaumbele
Matumizi ya
mara kwa mara na ya muda mmoja, kila aina ya matumizi , hata matumizi ya hiari.
kama bajeti yako inahusisha vitu vyote hivyo, kuna uwezekano mkubwa sana wa
wewe kutokuwa nje ya fedha, unaweza kusimamia fedha zako kwa kujiwekea bajeti
tu. kwa njia hii unaweza kuwekea kipaumbele matumizi yako
na kupanga fedha zako kwenye vitu vyenye umuhimu mkubwa sana kwenye
maisha yako. ni muhimu kuweka na kutoa umakini kwenye vitu vidogo ambavyo
vinaweza kuongezeka kwa kiasi kikubwa sana.
Kamwe usivipuuze vidogo vidogo au
mambo madogo, hakika najua unataka vyote, lakini weka vipaumbele kwenye vitu unavyovihitaji kwanza na vipi vya
kusubiria kwa ajiri ya baadaye, Na kutumia kutokana na utaratibu huo.
2. Boresha rekodi ya matumizi.
Unahitaji
kuangalia kwa makini na kwa karibu sana mahali fedha zako zinapokwenda na wapi hasa unaweza kukata pembe. magazeti ,Kunywa kahawa -vitu
vyote vinahesabiwa,haijalishi unatumia kiasi kidogo cha pesa, vyote
vinaongezeka na kuwa kiasi kikubwa sana, hivyo, unahitaji kufuatilia kila kitu.
njia bora na iliyo nzuri ni kudumisha rekodi ya matumizi .jaribu kuandika na
kuweka kumbukumbu juu ya vitu unavyotumia kwa zaidi ya mwezi. ukihusisha na
kila manunuzi. kama utaweza kufanya hivyo kwa muda mrefu sana, utaweza kupata
picha sahihi juu ya wapi hasa unatumia fedha zako na namna gani unaweza kupunguza na kuweza kukata kabisa gharama huko.
Katika Kuongeza na hili ,unaweza
kugawanya matumizi yako katika makundi mawili; mara kwa mara na yasiyo ya mara
kwa mara .hii itakusaidia kuwa na usimamizi wenye nguvu juu ya matumizi yako ya
mwezi.
3. Futa madeni yote.
Kama upo
kwenye madeni au unapambana kifedha, moja ya
njia rahisi sana kupambana na hali hii kutambaa kwenye magamba yako na
kupuuzia nakala yako ya benki na mahitaji ya malipo. lakini hili ,kwa
kutokuwa na maana, inaenda kufanya vitu
kuwa rahisi. badala yake ,kabili tatizo, jua unahitaji kushughulika na nini, Na
ushakapokuwa sahihi katika hili, utakuwa
na ufahamu wa hatua inayofuata. ni muhimu
madeni yako yawe madogo vyovyote vile unavyoweza bila ya kuikabili
biashara yako.
4.
Bima ni hatua ya kwanza.
Moja ya
hatua ya msingi kwa ajiri yako na kwa familia yako hapo baadaye ni bima. kuna
aina kadhaa za bima kama vile bima ya afya, bima ya ulemavu, bima ya umiliki wa
nyumba.
5.
Anzisha lengo la kuweka akiba na weka akiba mara kwa mara.
Jitazame
kwenye kioo na Kisha na useme hivi- Mwisho wa mwezi huu, utaweza kununua gari
ya ndoto yako kutoka kwenye akiba yako, Moja ambayo umekuwa ukiisubiri mno kwa
muda wote huo hii inakufanya hujisikiaje? msisimko? hakika! hii, kwa vyovyote
vile ,haitoweza kuwa kweli mpaka pale utakapokuwa na busara na kuanza kuweka
akiba fedha zako ili kufanikisha lengo lako. Jambo unalotakiwa kuliweka akilini
mwako pale unapokuwa unaweka akiba fedha yako ,Ni kuweka umakini juu ya nini
utaweza kufanya baada ya kuweza kufanikiwa kuweka fedha nyingi ,Ni muhimu kujua hizo fedha
unazoziwekea akiba utazitumia kwa ajiri ya nini, Utazifanyia nini? kuliko
kufikiria tu kuweka fedha zako pembeni.
Ni muhimu kuwa na malengo ya kujiwekea
akiba fedha zako. lakini watu wengi hawajui jinsi ya kuweka akiba fedha zao, kwa
hiyo, Unataka kuweka akiba ya fedha mara kwa mara lakini haujui cha kufanya?
Kama umeajiriwa;
Ingia akaunti ya kuweka akiba.
Weka
maelekezo yenye msimamo, ili kila mwezi fedha yako iweze kupata kusafirishwa
kwenye akaunti yako ya akiba moja kwa moja bila ya wewe kuwa na hofu kuhusu
fedha yako. Na kamwe usisubiri mpaka mwisho wa mwezi kwa ajiri ya hili. Kwani kuna
faida tatu za kufanya hivyo;
1.Fedha
inapata kusafirishwa kwenye akaunti yako ya akiba mapema sana pale unapolipwa
mshahara wako, kama umeajiriwa.
2. Kiasi
ulichoweka akiba kitaongezeka ikiwa utapata ongezeko la mshahara na pia utapata
Marejesho ya kiasi ushindani juu ya
akiba yako.
6. Tathimini uvumilivu wako wa
hatari.
Hatari
inafanya kazi kubwa sana, Na ya muhimu
kwenye kufanya maamuzi yote ya uwekezaji. kanuni ya shaba ni Inasema kwamba ,Kadri
marejesho yanavyokuwa makubwa kutoka kwenye baadhi ya Sehemu za uwekezaji, Ndiyo hatari inavyoweza kuhusika
kwa ukubwa zaidi. Baadhi ya sababu muhimu zinaoweza kukusaidia kuamua uvumilivu
wako wa hatari ni kama vile Mapato, matumizi,
malengo yako ya kifedha n.k.
kama unataka
kufanya maamuzi yenye busara Au Yenye hekima kwenye uwekezaji, Unahitaji
kutathimini uvumilivu wako wa hatari kabla ya kujiingiza kwenye kitu chochote
kile.
Moja ya kitu
kigumu sana kuhusu kusimamia na kuweka akiba fedha Ni hatua ya kwanza sana -kuanza.
hii inaweza kuwa ni vigumu sana kutumia akiba yako kwa busara ili kuelekea kwenye
malengo yako ya kifedha .
Mbinu zilizotajwa hapo juu zitakusaidia kwa kiasi
kikubwa sana kuendeleza mpango wa ukweli wa kuweka akiba na kuwekeza. zaidi ya
hapo, Zitakusaidia kuelewa mambo yanayohusiana na fedha kwa njia bora zaidi. Zifuate
Mbinu hizo na hakuna lolote lile litakalokuzuia kuweza kufanikisha mafanikio ya
kifedha. TUPO PAMOJA.
Geofrey
Mwakatika
Mwakatikageofrey@gmail.com. 0767382324.
0 comments:
Post a Comment