TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA MUONGOZAJI NDEGE DUNIANI KWA KUWAPIGA MSASA WANAHABARI KUHUSU TAALUMA YA UONGOZAJI NDEGE
Rais wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA), Shukuru Nziku akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kazi zinazofanywa na waongoza Ndege wakati wa siku ya Maadhimisho ya siku ya muongozaji ndege duniani iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa huduma za Uongozaji Ndege katika Kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Margareth Semkiwa na kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA), Sunday Walinda
Mkutano ukiendelea
Mkuu wa huduma za Uongozaji Ndege katika Kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Margareth Semkiwa akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusu huduma za kuongoza Ndege zinazotua, kuondoka na kutembea kwenye Uwanja ambapo huduma hii ufanywa kwa kuziona kwa macho wakati wa maadhimisho ya Maadhimisho ya siku ya muongozaji ndege duniani iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA), Godlove Longole( wa pili kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu njia zinazotumika kupitia Ndege angani kwenye ramani wakati wa maadhimisho ya Maadhimisho ya siku ya muongozaji ndege duniani iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa huduma za Uongozaji Ndege katika Kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Margareth Semkiwa akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusu huduma ya kuongoza Ndege zinazopanda na kushuka kwenye eneo linalozunguka Viwanja vikubwa ambapo wanatoa maelezo Maalumu kwa marubani kwa njia ya redio bila kuziona na baadhi ya Viwanja uziona kwa njia ya rada wakati wa maadhimisho ya Maadhimisho ya siku ya muongozaji ndege duniani iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA), Godlove Longole( wa pili kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu huduma ya kuongoza Ndege zinazopita kwenye anga la juu la nchi ya Tanzania pamoja na anga la chini lililoko mbali na Viwanja vya Ndege vinavyotoa huduma ya kuongoza Ndege wakati wa maadhimisho ya Maadhimisho ya siku ya muongozaji ndege duniani iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waongozaji wa Ndege katika Kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakiwa kwenye picha ya pamoja
Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA) kimeshiriki maadhimisho ya siku ya muongozaji ndege duniani kwa kutoa elimu kuhusu kazi za ungozaji ndege kwa waandishi wa Habari leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Rais wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA), Shukuru Nziku amesema malengo ya chama hicho ni kuwaweka pamoja wanachama ili kuendana na wakati pamoja nakuwapeleka wanachama hao kwenye mafunzo pamoja na kuwahamasisha kujisomea ili kuendana na wakati.
Amesema lengo chama hicho kwa mwaka huu ni kuwatumia waandishi wa Habari ili kuweza kukitangaza chama hicho ili kiweze wa kuwafikia wananchi mbalimbali pamoja na kutoa elimu kwa wanafunzi waweze kupenda taaluma hiyo.
Amesema kwa kipindi cha nyuma Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ulikuwa na uwezo wa kupokea Ndege 230 kwa siku lakini kutokana na changamoto ya Uviko-19 kwa sasa wanapokea Ndege chini ya 150 kwa siku na Ndege zinazopita kwenye anga la Dar es Salaam kwa siku ni zaidi ya 249na Ndege hizi mara nyingi zinatokea Afrika Kusini kwenda Misri au kutokea Misri kwenda Afrika Kusini.
Pia amesema baada ya kuwepo kwa Sheria ya usimamizi wa Ndege zisizokuwa na rubani imeweza kusaidia kuondoa changamoto hasa kwa waongoza Ndege hivyo kupelekea kuimarisha usimamizi wa Viwanja na wadau mbalimbali kuendelea kusimamia Sheria iliyowekwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Akizungumzia changamoto za kazi hiyo ni kuwa na maamuzi ya haraka na ambayo ni sahihi ili kuweza kutatua matatizo mbalimbali yanayotokea nje na ndani ya Ndege pamoja na ugomjwa wa Uviko 19 umesababisha wafanyakazi wengi kudumaa kutokana na upungufu wa Ndege kutokana na nchi mbalimbali kufunga nchi hivo hivyo wafanyakazi hawafanyi kazi kihufasaha.
Huu ni mwaka wa 60 tangu kuanzishwa rasmi kwa chama cha uongozaji ndege duniani kinachoitwa International Federation of Air Traffic Controllers' Associations (IFATCA) chenye makao makuu nchini Canada.
0 comments:
Post a Comment