Wednesday, 3 November 2021

TANZANIA NA UBELGIJI WATIA SAINI HATI YA MAKUBALIANO YA BIASHARA YA USAFIRI WA ANGA

 


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano ya kibiashara ya usafiri wa anga kati ya Tanzania na Ubelgiji.



Balozi wa Ubelgiji nchini Balozi, Peter VAN ACKER akisisitiza umuhimu wa ushirikiano huo wakati wa hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano ya kibiashara ya usafiri wa anga kati ya Tanzania na Ubelgiji.



Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Mhandisi. Aron Kisaka akisioma taarifa ya ushirikiano baina ya Tanzania na Ubelgiji  katika hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano ya kibiashara ya usafiri wa anga kati ya nchi hizo mbili.




Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S. Johari akisisitiza jamba wakati hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano ya kibiashara ya usafiri wa anga kati ya Tanzania na Ubelgiji.


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Kulia) na Balozi wa Ubelgiji nchini Balozi,  Peter VAN ACKER (Kushoto) wakitia saini hati ya makubaliano ya kibiashara ya usafiri wa anga kati ya nchi hizo mbili.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Kulia) na Balozi wa Ubelgiji nchini Balozi, Peter VAN ACKER (Kushoto) mara baada ya kusaini hati ya makubaliano ya kibiashara ya usafiri wa anga kati ya nchi hizo mbili.



Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa na Balozi wa Ubelgiji nchini Balozi,  Peter VAN ACKER wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya Anga mara baada ya kusaini hati ya makubaliano ya kibiashara ya usafiri wa anga kati ya nchi hizo mbili.

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa amesaini makubaliano ya kibiashara na Balozi wa Ubelgiji hapa nchini.

Makubaliano hayo yatawezesha huduma ya biashara za ndege kati ya Tanzania na Ubelgiji ambapo sasa ndege za Tanzania zitaweza kwenda moja kwa moja Ubelgiji na ndege za Ubelgiji kuja Tanzania.

Akiongea katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dodoma Prof. Mbarawa ameyataka mashirika ya ndege kuanza fursa hiyo muhimu ili kuwekeza na kuimarisha fursa za uchumi hususani katika nyanja za utalii na biashara.

“Huu ni mwanzo tu, tumejipanga kuhakikisha sekta ya usafiri wa anga inafunguka na kuwaleta wadau wengi wa maendeleo nchini na sisi kutoka kwenda kuangalia fursa huko ziliko”. amesisitiza Prof. Mbarawa.

Naye Balozi wa Ubelgiji hapa nchini Balozi, Peter VAN ACKER amesema chini ya mpango huo, ndege za Tanzania zitakwenda moja kwa moja Ubelgiji na ndege kutoka Ubelgiji zitakuja moja kwa moja Tanzania zikitua katika Viwanja vya Ndege vya Kimataifa vya Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro (KIA)  na Abeid Amani Karume (AAKIA).

Kaimu Katibu Mkuu (Sekta ya Uchukuzi) handisi. Aron Kisaka ameeleza kuwa Wizara imejipanga kikamilifu kuhakikisha Tanzania inanufaika vyema na fursa zitakazotokana na makubaliano haya muhimu.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S. Johari ameelezea kufarihishwa na makubaliano yaliyofikiwa na nchi hizi na kueleza kuwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini itaendelea kutafuta fursa kama hizi ili kuifungua Tanzania duniani.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA