Monday 11 October 2021

TCAA YAKUTANA NA WADAU WA NDEGE ZISIZO NA RUBANI ZANZIBAR

 


Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria TCAA Bi. Clara Mpili akitoa neno la ukaribisho kwa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar Bw. Fadhil Juma Ali katika mkutano wa wadau wa ndege zisizo na rubani-Zanzibar




Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria TCAA Bi. Maria Memba akifafanua kuhusu kanuni na taratibu za kumiliki na kuendesha ndege zisizo na rubani-Zanzibar


Meneja wa TCAA Zanzibar Bw. Mbarouk Khamis Hamad akieleza jambo kwa wadau wa ndege zisizokuwa na rubani wakati wa semina elekezi iliyoandaliwa na TCAA Zanzibar

Wadau wa ndege nyuki wakiendelea na semina elekezi iliyofanyika Zanzibar


Mkaguzi wa ndege zisizo na rubani kutoka TCAA Bw. Ibrahim Abdallah akiwasilisha mada ya ufahamu wa ndege zisizo na rubani kwa wadau wa ndege hizo Zanzibar


Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar Bw. Fadhil Juma Ali (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi kutoka TCAA pamoja na wadau wa ndege nyuki- Zanzibar


Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imetoa semina elekezi kwa wadau wa ndege zisizo na rubani (Drones) kuhusu uelewa wa Sheria, Kanuni na Taratibu za kumiliki na kuendesha ndege hizo.

Semina hiyo ya siku tatu imefanyika Zanzibar kuanzia tarehe 7-9, 2021 na kuhusisha wadau mbalimbali ikiwemo Idara ya Uhamiaji Zanzibar, Kamisheni ya Utalii, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Polisi, TRA-Zanzibar, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar pamoja na wamiliki na waendesha ndege zisizo na rubani Zanzibar.

Aidha, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria TCAA Bi. Maria Memba amesema kanuni za uendeshaji wa ndege zisizo na rubani zimeanza kutumika tangu mwaka 2020, hivyo amesisitiza kuwa ni muhimu zikafuatwa ili kulifanya anga letu liendelee kuwa salama kwa watumiaji wote yaani ndege zenye rubani na zisizokuwa na rubani

Bi. Memba ameongeza kuwa, kanuni na taratibu za uendeshaji wa ndege zisizo na rubani zinapatikana katika tovuti ya TCAA inayopatikana kwa anwani www.tcaa.go.tz 


0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA