MORRISON AIBWAGA YANGA CAS
MCHEZAJI wa Kimataifa wa Ghana anayecheza Klabu ya Simba, Bernard Morrison ameshinda kesi yake dhidi ya Yanga SC, kesi iliyokuwa ikisikilizwa na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS). Taarifa iliyotolewa na Mahakama hiyo imeeleza kuondoa rufaa iliyowasilishwa na Klabu ya Yanga dhidi ya Mchezaji huyo raia wa Ghana anayecheza nchini Tanzania.
CAS wameeleza kuwa kesi hiyo ilitolewa maamuzi na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) Agosti 12, 2020. Imeelezwa kuwa mkataba wa awali wa Morrison uliisha Julai 14, 2020, Morrison alilazimika kulipa kiasi cha fedha Dola za Marekani (USD 30,000) baada ya kushindwa kusaini mkataba wa pili na Yanga SC.
Yanga SC walipeleka suala hilo CAS wakidai kulipwa kiasi cha USD 200,000 baada ya Mchezaji huyo kuvunja mkataba na Klabu hiyo. Mahakama ya CAS ilikaa Julai 29, 2021 na kutupilia mbali rufaa ya Yanga SC ikidaiwa haina mashiko.
0 comments:
Post a Comment