Wednesday 31 May 2023

MULIKA TANZANIA YAZIDI KUWAFIKA MACHINGA NA KUWAJENGEA UWEZO

 

Taasisi ya Mulika Tanzania imewajengea uwezo kwa kundi maalumu la Wamachinga  15 kwa ajili ya uainishaji wa vituo vya Afya vinavyotoa huduma ya Afya ya Uzazi katika Wilaya ya Temeke.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Afisa Vijana wa Wilaya ya Temeke Anne Marica amesema sasa ni wakati wa vijana kufanya maamuzi yaliyo sahihi hasa kwenye suala la Afya ya Uzazi ili kuweza kuendana na sera ya Taifa ya maendeleoya vijana ya mwaka 2007.

Amewasisitiza kuandaa Taarifa halisi ili kuweza kuendana na uhalisia wa hasa kwenye elimu ya Afya ya Uzazi na namna ya kupata Taarifa sahihi kwenye vituo vya Afya vilivyopo katika Wilaya ya Temeke.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Mulika Tanzania Bw. Hussein Melele amesema leo lengo kubwa ni kuviainisha vituo vya Afya vinavyotoa huduma ya Afya ya Uzazi katika Wilaya ya Temeke ili kuweza kwenda kupata Taarifa za vijana ili kuona ni kwa namna gani wanaweza kutatua changamoto ya vijana kwenda au kutokwenda kwenye vituo vya Afya.

Huu ni muendelezo wa programu ya IMARIKA ambayo sasa ipo katika awamu ya pili, na tayari wachuuzi wa mitaani zaidi ya 70 wamepewa taarifa za kina na mwongozo wa kupata mikopo kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGA) na katika kuweka muendelezo wa elimu hii, wachuuzi 15 walichaguliwa na kuwezeshwa na maarifa muhimu ili kuwa Wakufunzi wa Wakufunzi (ToT) kwa lengo kuwawezesha kuongoza na kusaidia wengine kwa ufanisi katika shughuli zao za kila siku.

Katika kuutekeleza mradi huu, Mulika Tanzania inashirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), na miongoni mwa mambo yanayotekelezwa ni kutoa elimu ya afya ya uzazi, stadi za maisha elimu, na ushiriki wa vijana katika maeneo ya uongozi yaliyolengwa mahususi kwa wafanyabiashara ndogo ndogo wa mitaani, wanaojulikana kwa jina la "Machinga," katika Wilaya ya Temeke Dar-es-Salaam.



Afisa Vijana wa Wilaya ya Temeke Anne Marica kitoa ufafanuzi kuhusu namna ya kutafuta Taarifa kwenye vituo vya Afya kwa kundi maalumu la Wamachinga waliojengewa uwezo (ToT) wanakutana kwa ajili ya uainishaji wa vituo vya Afya vinavyotoa huduma ya Afya ya Uzazi katika Wilaya ya Temeke wakati wa semina iliyoandaliwa na Taasisi ya Mulika Tazanania na kufanyika katika ofisi za Taasisi hiyo iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Mulika Tanzania Bw. Hussein Melele akizungumza kuhusu namna watakavyoweza kuviainisha vituo vya Afya vinavyotoa huduma ya Afya ya Uzazi katika Wilaya ya Temeke wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo kwa kundi maalumu la Wamachinga  15 yaliyifanyika katika ofisi za Taasisi hiyo iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mfanyabiashara mdogo Rajabu Kindamba akitoa maelezo kuhusu maswali watakayokwenda kuuliza wakati warsha ya kuwajengea uwezo kwa kundi maalumu la Wamachinga  15 watakavyoweza kuviainisha vituo vya Afya vinavyotoa huduma ya Afya ya Uzazi katika Wilaya ya Temeke 
Mfanyabiashara mdogo Winnie Hisluck akizungumza namna watakavyokwenda kutafuta Taarifa wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo kwa kundi maalumu la Wamachinga  15 watakavyoweza kuviainisha vituo vya Afya vinavyotoa huduma ya Afya ya Uzazi katika Wilaya ya Temeke.
Mratibu wa mradi wa Imarika, Winfrida Mponzi akitokea ufafanuzi maswali yatakayoulizwa kwenye vituo vya Afya vinavyotoa huduma ya Afya ya Uzazi katika Wilaya ya Temeke wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo kwa kundi maalumu la Wamachinga  15 iliyofanyika katika ofisi za Taasisi hiyo iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Picha ya pamoja 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA