Wednesday, 3 May 2023

NJIA 5 ZA KUWEZA KUSAHAU MATUKIO YENYE KUUMIZA SANA NA KUHUZUNISHA SANA



NB: Zingatia kwamba chochote ambacho utafanya au kusema hakiwezi kumfurahisha kila mtu au kumridhisha kila mtu hivyo fuata ujumbe mpaka mwisho kuelewa kwa undani

Kila mtu yupo na kumbukumbu za matukio yenye kushtua sana na kuhuzunisha sana ambapo kwa njia moja au nyingine kila mtu hutumia njia zake kukabiliana na kumbukumbu hizo.


Zipo njia sahihi na vilevile zipo njia zenye kuleta madhara zaidi kuliko ufumbuzi wake.

Matukio ambayo husababisha kumbukumbu mbaya ni kama vile kifo cha mzazi au mlezi au mtu yeyote ambaye unampenda sana,ajali,kutekwa nyara, ugomvi wa wazazi,kupitia manyanyaso kutoka kwa watu wengine n.k


Kabla ya kujua njia 6 za kusahau matukio hayo tuangalie namna ambavyo matukio hayo yameathiri uwezo wako wa kufikiria.

Katika Mawazo Yako Andika NDIYO au HAPANA kulingana na hali yako ya sasa.


1.Ninaamini matatizo yangu yote chanzo ni watu wengine na siwezi kufanya chochote kukabiliana na hali yangu ya sasa?

2.Ninaamini matendo yangu hayana athari zozote kwa watu wengine.Matendo yangu hayawezi kuleta majeraha au maumivu kwa watu wengine?

3.Ninaamini siwezi kufanya kitu  chochote chenye kwenda tofauti na matakwa yangu ?

4.Ninaamini sina fedha,sina muda,za kutumia kufanya kitu chochote pale ambapo watu wengine wanataka nifanye ?

5.Ninaamini huwa ninapata maumivu mwilini ili nisifanye kazi,na huwa sina nguvu za kufanya kazi 

6.Ninaamini siwezi kuishi kwa kufuata taratibu na sheria za eneo ninapoishi naona ni sahihi kusema nimesahau au kupuuza majukumu yangu ?

7.Ninaamini watu wengine wanatakiwa kufuata maagizo yangu nikitaka wafanye hata kama hawaelewi sababu za mimi kutoa maagizo?

8.Ninaamini nipo na haki ya kutumia mali za watu wengine vile ninavyotaka bila ruhusa zao?

9.Ninaamini watu wengine wamekuwa wananigeuka na kunisaliti hivyo siwezi kuamini mtu yeyote?

10.Ninaamini ninaweza kufanya maamuzi bila kujua taarifa zozote?

11.Ninaamini nipo sahihi na hoja zangu zote zipo sahihi hata kama utatolewa ushahidi kuonyesha sipo sahihi bado nitadai nipo sahihi?

12.Naamini natakiwa kushinda tu siku zote, naamini kupanga namna ya  kuendesha maisha hakuna umuhimu wowote?

13.Naamiini hofu ni udhaifu mkubwa sana hivyo ninakataa kuwa na hofu hata kama nipo na hofu kubwa?

14.Ninaamini kuonekana mwenye hasira kupita kiasi,kufoka, kutukana, kutoa vitisho ni njia nzuri sana ya kupata mahitaji yangu kutoka kwa watu wengine?


Kama umejibu NDIYO maswali mengi maana yake kumbukumbu za matukio yenye kushtua sana na kuhuzunisha sana yameathiri uwezo wako wa kufikiria na yamekuwa chanzo cha mahusiano yako na watu wengine kuwa na ugomvi wa mara kwa mara.


MATUKIO YENYE KUUMIZA SANA NA KUHUZUNISHA SANA YAPO KAMA IFUATAVYO

Matukio yenye kushtua sana na kuhuzunisha sana yapo katika makundi mawili utotoni na ukubwani 

a.MATUKIO YA UTOTONI

Matukio ya utotoni ni kama vile

Manyanyaso ya kimwili na kihisia, kupuuzwa kimwili na kihisia,ugomvi wa wazazi,kuishi na mtu mlevi kupindukia au mgonjwa sana,kuishi na mtu ambaye alifungwa gerezani mara kwa mara.Ufafanuzi jibu maswali yafuatayo kwa kuandika NDIYO au HAPANA

1. Je mzazi wako au mtu mkubwa kwako nyumbani kwenu mara kwa mara alikuwa anakufokea, kukutukana, kukupa vitisho,kukujibu vibaya sana,kukufanya uwe na hofu ya kuumizwa kimwili?


2. Je mzazi wako au mtu mkubwa kwako nyumbani kwenu mara kwa mara alikuwa akikupiga, kukusukuma,kukupiga vibao,kukurushia vitu vyenye kudhuru mwili,alikupiga sana mpaka ulipata makovu au majeraha ? 


3. Je mtu mkubwa kwako au ambaye anakuzidi miaka 5 nyumbani kwenu mara kwa mara alikuwa akishika mwili wako kwa njia ya kukutaka kimapenzi?


4. Je umekuwa ukiishi nyumbani kwenu na kuhisi kuwa hakuna mtu yeyote nyumbani kwenu anaona fahari kuishi na wewe au hakuna mtu ambaye anakupenda? Je ndugu zako hawapendani ,hawana ushirikiano,hawana mahusiano mazuri,hakuna mwenye kumsaidia mwenzake ?


5. Je mara nyingi ulikuwa hupati chakula,ulivaa nguo chafu, kutembea bila viatu,ulikosa mtu wa kukulinda na kukutetea,ulikosa mtu wa kusikiliza maumivu yako ? Je wazazi wako walikuwa wagonjwa sana au ulipokuwa ukiugua mara kwa mara hukupelekwa hospitali?


6. Je mam yako au mama yako mlezi mara kwa mara uliona anapigwa, kufokewa, kutukanwa, kudhalilishwa,kupigwa vibao, kubamizwa ukutani, kurushiwa vitu vyenye kudhuru mwili,alipigwa ngumi,kukabwa shingoni,kupigwa kitu kizito mwilini,je mama yako au mama wa kambo aliwahi kutishiwa silaha? 


7. Je ulipokuwa mdogo uliishi na mtu ambaye alikuwa mlevi kupindukia,mwenye  kutumia bangi au dawa za kulevya?


8. Je utotoni mwako umeishi na mtu nyumbani ambaye alikuwa na huzuni kupita kiasi msongo wa mawazo,mgonjwa wa akili ambaye aliwahi kupelekwa hospitali kwa matibabu ya ugonjwa wa akili?

Je kuna mtu yeyote nyumbani kwenu alijaribu kujiua bila mafanikio?


9. Je ulipokuwa mdogo wazazi wako walitengana au walikuwa wanaishi sehemu tofauti au walipeana talaka ?

10. Je katika nyumba yenu kuna mtu alifungwa jela au alikuwa anafungwa jela na kutoka kisha anafungwa tena ?


Kama umejibu NDIYO maswali 4 utakuwa hatarini kupata changamoto zifuatazo za kiafya kuumwa kichwa na mgongo, tumbo kuvurugika, moyo kwenda mbio, kizunguzungu,kupata maambukizo ya magojwa ya bakteria na virusi, madonda tumbo, uvimbe, kupooza, shinikizo la damu, kuugua muda mrefu sana bila kupata nafuu,kuugua mara kwa mara na ikiwa umejibu NDIYO maswali 6+ utakuwa hatarini kujiua ,utakuwa hatarini kupata saratani, uvimbe, matatizo ya mapafu,figo,ini, kuvunjika mifupa,ugonjwa wa moyo,kupata maambukizo ya magojwa kama ukimwi na vilevile utakuwa hatarini kuumwa sana kichwa na mgongo.


Kama umejibu NDIYO maswali 6+ utakuwa hatarini kuanza matumizi ya pombe kupindukia,bangi , kutumia fedha nyingi sana ghafla, kucheza kamari, uraibu wa pornography,kuvunja mahusiano mara kwa mara,kugombana mara kwa mara na watu wengine


MATUKIO YENYE KUUMIZA SANA NA KUHUZUNISHA SANA UKUBWANI NI

Ukubwani unaweza kukumbana na matatizo mbalimbali kama vile kutekwa nyara,kubakwa au ulawiti,ajali yenye kusababisha ulemavu wa kudumu, kufukuzwa kazi,kupigwa sana , kunusurika kuuawa, kumfumania mwenza wako,kifo cha mtu unampenda sana, kushambuliwa kwa maneno makali sana,kupitia ubaguzi, kutengwa,n.k ambayo msingi mkubwa wa maumivu huwa ni kumbukumbu za utotoni.


Kutokana na matukio hayo utaona mabadiliko yafuatayo mwilini


VIASHIRIA VYA MSONGO WA MAWAZO AMBAO HUTOKANA NA KUMBUKUMBU ZA MATUKIO YENYE KUUMIZA SANA

a.Kuanza kulia, kuhuzunika mara kwa mara, hasira kupita kiasi,moyo kwenda mbio sana, kizunguzungu, kichefuchefu, miguu kuishiwa nguvu, tumbo kuvurugika, kutetemeka sana,


b.kujuona hauna thamani, kujichukia kupita kiasi, kutamani kujiua, kupoteza kumbukumbu,kujuta sana, kujikosoa sana,uchovu kupita kiasi,kula sana au kushindwa kula kabisa 


c.kukata tamaa ya maisha,kuogopa sana mwanga mkali,harufu,sauti kali ,kutafuna meno,kukosa utulivu, kujitenga sana, kuchanganyikiwa haraka sana,hofu ya kitu kibaya kutokea ghafla


d.kupoteza hisia za mapenzi,kukosa huruma kwa mtu yeyote,kutamani kulipa kisasi,kubeba chuki moyoni muda mrefu sana,kushindwa kusamehe makosa yako


e.Kujiona kituko,kujiona kitu cha aibu mbele za watu, kupaniki,kifua kubana sana.

Kukwepa mada,kukwepa watu,kukwepa maeneo yenye kukumbusha matukio yenye kushtua sana na kuhuzunisha sana 


NJIA 6 ZA KUSAHAU MATUKIO YENYE KUUMIZA SANA NA KUHUZUNISHA SANA

Kwanza kabisa huwezi kusahau matukio hayo na juhudi zozote za kusahau matukio hayo huzidisha maumivu makali sana kuliko mwanzo.

Njia za kukabiliana na hali hiyo ni

1.PATA UTULIVU WA AKILI

Utulivu wa akili unaweza kuupata kwa njia zifuatazo

a.Osha uso wako na mikono  kwa maji ya baridi,

b.Fanya mazoezi mepesi mepesi ya viungo

c.Kukumbatia mwili wako mwenyewe utazalisha homoni za Oxytocin zenye kufanya uhisi umekumbatiwa na mtu unampenda sana au kupapasa sehemu za mikono na,mabega kifua kama kufanya massaging

d.Kupiga miayo kwa nguvu kuruhusu hewa kuingia kwa wingi sana kifuani

e.kutumia lavender

F.Vuta pumzi polepole kisha hesabu 1-5 kisha ruhusu hewa kutoka kifuani ukihesabu 1-5 mpaka mapigo ya moyo yarudi chini

g.Vuta pumzi kwa nguvu zote kupitia puani .Fanya zoezi hilo kwa dakika 5 hakikisha kifua kinabonyea wakati kuvuta pumzi ndefu


2.FANYA MAZUNGUMZO

Kuzungumza na mtu ambaye unamuamini ,zungumza kuondoa mzigo kifuani.Kama upo na kitu chochote chenye kuumiza kichwa chako tafuta mtu wa kusikiliza maumivu yako utaona mzigo kifuani unaondoka na unakuwa mwepesi


3.Andika matukio yenye kushtua sana na kuhuzunisha sana ambayo umepitia kisha eleza maumivu makali sana ambayo unapitia kwa maandishi

4.UNAWEZA KUTUMIA MAUMIVU YAKO KUFANYA SANAA- Unaweza kuandika shairi n.k kama kumbukumbu za matukio fulani unaandika kwa hisia kali sana maumivu yanaondoka haraka sana 


5.TUMIA MAUMIVU HAYO KAMA HAMASA YA MAFANIKIO 

Ukiumizwa tumia fursa hiyo kuacha alama kwa kizazi kipya,itasaidia kufurahia maumivu badala ya kuchukia maumivu hayo


Kama tatizo lako ni kubwa zaidi tunaweza kuwasiliana kwa  ajili ya Counselling session na ufafanuzi wa kilichoandikwa hapo juu na utaona mabadiliko na kujisikia nafuu ndani ya muda mfupi baada ya mazungumzo.

Kwa wapenzi wa  kusoma vitabu unaweza kupata nakala zangu orodha ipo chini ๐Ÿ‘‡

Kupata kitabu cha

1.UTULIVU WA AKILI KIPINDI KIGUMU (Softcopy)

2.FIKRA ZAKO FURAHA YAKO (softcopy)

3TIBA YA MSONGO WA MAWAZO (by & Softcopy) 

5.MALEZI YA UBONGO KISAYANSI( hardcopy & softcopy)

6.TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA (Hardcopy & softcopy)


7.MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE (hardcopy &softcopy)


BEI Kitabu kimoja softcopy 5000 , hardcopy moja 10000


Mawasiliano 

+255766862579

+255622414991

Imeandikwa na 

Said Kasege

Temeke,Dar es salaam

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA