TCAA YATOA MKONO WA PASAKA KITUO CHA KULELEA WATOTO CHA ZILI
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imekabidhi mahitaji kwa kituo cha kulea watoto cha ZILI kilichopo Kipawa Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kurejesha kwa jamii inayowazunguka.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mahitaji hayo yaliyogharimu kiasi cha Shilingi (TSHS) Milioni Moja, Afisa Habari na Mawasiliano wa TCAA Bi. Maureen Swai amesema Mamlaka imeguswa kutoa mkono wa Pasaka kwa kituo hiki ambacho kinalea watoto kumi kwa sasa.
Mkurugenzi wa kituo cha ZILI Bw. Emanuel Zadock ameishukuru TCAA kwa kuguswa kuwashika mkono wakati huu na kuwaomba wadau wengine kuendelea kuvishika mkono vituo vinavyowatunza watoto wenye mahitaji kwani ni baraka kubwa sana.
Afisa Uhusiano na Mawasiliano - TCAA Maureen Peter Swai(kushoto) akikabidhi msaada kwa Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto cha Zili House Bw. Emanuel Zadock (kulia) ikiwa ni kurudisha kwenye jamii kwakusambaza upendo na tabasamu kwa watoto yatima wa kituo hicho kilichopo eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam. Msaada uliotolewa na TCAA ni mchele, Unga, mafuta ya kula, Taulo za Kike, sabuni, ngano nk.
Afisa Uhusiano na Mawasiliano - TCAA Bi. Maureen Swai akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada katika kituo cha kulelea watoto cha Zili ikiwa ni kurudisha kwenye jamii kwakusambaza upendo na tabasamu kwa watoto yatima wa kituo hicho hasa kwa kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka.
Dorethea Daniel akitoa neno la shukrani wa viongozi pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa kuweza kuwapatia msaada kituo hicho kilichopo eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) pamoja na watoto wakisikiliza historia ya Kituo cha kulelea watoto cha Zili House wakati wa hafla ya kutoa msaada katika kituo hicho
Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Kituo cha Zili House pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho mara baada ya kukabidhi msaada ikiwa ni kurudisha kwenye jamii kwakusambaza upendo na tabasamu kwa watoto yatima wa kituo katika kituo hichokilichopo eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment