Showing posts with label NYERERE. Show all posts
Showing posts with label NYERERE. Show all posts

Sunday, 16 October 2016

UVCCM MUFINDI WATAKA MWALIMU NYERERE AENZIWE KWA VITENDO

Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani Iringa kwaridela vijana wa cahama cha mapinduzi wilayani Mufindi wakati wa sherehe siku ya vijana wa chama cha mapinduzi

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi Yohannis Kaguo kushoto akiteta jambo na katibu mkuu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa Hassani Mtenga wakati kukagua mabanda ya maonyesho yaliyofanyika katika ofisi za CCm wilaya ya Mufindi
Katibu wa UVCCM Mufindi Fatuma Ngailo na mwenyekiti wa vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Mufindi felix Lwimbo wakielekea kufanya usafi katika hospitali ya mafinga
Hawa ni baadhi ya vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Mufindi wakiwa wamemaliza kufanya usafi katika hospital ya mji wa Mafinga wakiongozwa na katibu msaidizi wa mufindi.

   Na fredy mgunda,iringa


VIJANA wa chama cha mapinduzi (CCM)wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa wamewataka wafanyakazi na viongozi wa serikali kufanya kazi kwa kujituma ili kumuenzi mwalimu Nyerere kwa vitendo.

Haya yalisemwa na katibu wa UVCCM Mufindi Fatuma Ngailo wakati akisoma lisala kwa mgeni rasmi wakati wa maazimisho ya siku ya vijana wa chama cha mapinduzi yaliyofanyika wilayani Mufindi.

Viongozi wa vyama vya Siasa wametakiwa kuiga kwa vitendo uzalendo na moyo wa kujitoa aliokuwa nao Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake ili kuliwezesha Taifa kupiga hatua kimaendeleo.

“nitahakikisha nazilinda mali za taifa,nasisitiza uwajibika,uzalendo,uandilifu na nidhamu katika kulitumikia taifa la Tanzania kama unakumbuka mwalimu alikuwa anapenda kutumia neno (it can be done play your part) kila mtu atimizi majukumu yake” Alisema Ngailo

Amesema kuwa kumbukumbu za Baba wa Taifa zilizohifadhiwa vizuri katika makumbusho hiyo zina mambo mengi ya kujifunza ambayo wanasiasa wanatakiwa kuyafanya kwa vitendo hasa uzalendo kwa nchi, uvumilivu, upendo na moyo wa kujitoa kwa dhati kuwatumikia wananchi.

“Kupitia kumbukumbu hizi sisi vijana tumejifunza ukomavu wa demokrasia aliokuwa nao Mwalimu Nyerere akiwa ndani na nje ya Bara la Afrika,wengi wanadhani Demokrasia ni wakati wa uchaguzi tu, kumbe demokrasia ni pamoja na kuheshimu watu wengine” Alisema Ngailo

Akiongea kwenye sherehe hizo mwenyekiti wa vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Mufindi felix Lwimbo Alieleza kuwa maisha aliyoishi Baba wa Taifa ni mfano wa kuigwa na viongozi na watanzania wote hasa pale alipojitofautisha na viongozi wengi wa Bara la Afrika alipoepuka tamaa ya madaraka na mali kwa manufaa ya taifa.

“Sote ni mashahidi kupitia kumbukumbu zake tumeona mahali alipokuwa anaishi mwalimu kabla hajajengewa nyumba na Jeshi kama Rais mstaafu wengi walitegemea asingeishi katika eneo lile, kumbukumbu hii nzuri aliyoiacha inatufundisha watanzania kuwa mwalimu aliitanguliza Tanzania mbele kuliko maslahi yake binafsi” Amesisitiza Lwimbo

Lwimbo amebainisha kuwa serikali itaendelea kumuemzi Baba wa Taifa kwa yale aliyoyafanya na kuyasimamia kwa manufaa ya taifa huku akitoa wito kwa viongozi wa vyama vya Siasa wawe na kiasi na waridhike na vile walivyonavyo.

“Suala la kuridhika na kuwa na kiasi linapaswa kuzingatiwa, wanasiasa wanapaswa kuwaheshimu wananchi wanaowachagua kupitia chaguzi mbalimbali, matokeo yanapotoka kama ni sahihi basi wanasiasa wakubaliane na maamuzi yao” Ameainisha Lwimbo

Lwimbo amemalizia kwa kuwataka watendaji wote wa serikali ya wilaya ya Ileje kufanya kazi kwa uaminifu,uadilifu,kuwajibika kwenye majukumu yao na kujituma na kamwe hata kuwa tayari kuwavumilia watendaji ambao ni wazembe kazini.

Kwa upande wake katibu wa CCM mkoani Iringa Hassani Mtenga ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi katika sherhe hizo alisema kuwa watanzania wanayo mengi ya kujifunza kupitia vitu alivyoviacha Baba wa Taifa ambavyo vimehifadhiwa katika Makumbusho hiyo.

Amesema kuwa maisha ya uadilifu aliyoishi enzi za uhai wake na mchango wake katika kuiletea maendeleo Tanzania na Bara la Afrika vinapaswa kuenziwa kwa nguvu zote na viongozi wa Tanzania.

“kwa wale mliopata nafasi ya kuitembelea makumbusho na jua mmejifunza vitu vingi kumhusu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwamba alikuwa ni mtu wa namna gani kwa viwango vya Afrika na dunia kutokana na kumbukumbu ya uadilifu aliyoiacha ndani na nje ya mipaka ya Tanzania” alisema Mtenga

Naye mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi Yohannes Kaguo aliwataka vijana kuacha kulalamika kwa kukosa ajira kutoka na mfumo wa serikali na kuwaomba wajitume na kuwa wabunifu ili waweze kujiajiri wenyewe.

“Saizi unakuta vijana wengi wanashinda mitaani na kupiga siasa tu na sio kupanga mipango ya kutatua changamoto zao za kimaendeleo ,saa moja asubuhi unawakuta vijana kwenye mabao,pooltable na draft sasa unafikiri hapo utapata maendeleo”alisema Kaguo

Saturday, 15 October 2016

KILIMANJARO WAADHIMISHA MIAKA 17 YA KUMBUKUMBU CHA KIFO CHA BABA WA TAIFA KWA KUOTESHA MITI

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki akiongozana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru wakati alipowasili katika chanzo cha maji cha Shiri kwa ajili ya zoezi la kuotesha miti ikiwa ni kuadhimisha miaka 17 ya kifo cha Baba wa Taifa ,Hayati Mwl Julius Nyerere.
Wakuu wa wilaya za Hai na Moshi ,Gelasius Byakanwa (wa pili toka kulia) na Kippi Warioba (wa tatu toka kushoto waliungana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro katika zoezi hilo.kulia ni Katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Aisha Amour.
Eneo lilipo jirani na chanzo cha maji cha Shiri ambalo liliandaliwa kwa ajili ya kuoteshwa miti.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiki akizungumza kabla ya kuanza kwa zoezi la uoteshaji miti.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki akiotesha mti katika eneo la chanzo cha maji la Shiri Njoro lililopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akiotesha mti katika eneo hilo.
Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro,Aisha Amour akiotesha mti katika eneo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kipi Warioba akiotesha mti katika eneo hilo zoezi ambali lilishirikisha watumishi wa idara mbalimbali za serikali na wafanyakazi wa Mamlaka ya Majsafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA).
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akiotesha mti katika eneo hilo.
Baadhi ya watumishi wa idara za serikali wakishiriki katika zoezi hilo.
Meneja Biashara wa MUWSA,John Ndetiko akiotesha mti katika eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki akiongozana na viongozi wa wilaya pamoja na wananchi wengine kutembelea chanzo cha maji cha Shiri Njoro .
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa(kushoto) Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba (anayefuatia pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro wakitizama eneo ambalo kunafanyika mgawanyo wa maji katika chanzo cha maji cha Shiri Njoro.
Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba (kulia) akiwa pamoja na Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa.
Chanzo cha maji cha Shiri.
Baadhi ya watumishi wa serikali wakitizama chanzo cha maji cha Shiri njoro.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Said Meck Sadiki akizungumza katika chanzo hicho.
Meneja Biashara wa MUWSA ,John Ndetiko akizungumza katika chanzo hicho.
Mkuu wa mkoa akijiadaa kuvuka katika eneo lenye maji katika chanzo hicho.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA