Showing posts with label USAFI. Show all posts
Showing posts with label USAFI. Show all posts

Wednesday, 7 June 2017

GREEN WASTEPRO LTD WASHIRIKI WIKI YA MAZINGIRA KWA KUSAFISHA FUKWE YA AGA KHAN


Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akisitiza jambo kwa wadau walioshiriki zoezi la usafi katika fukwe ya bahari ya Hindi eneo la Aga Khan na kuwaomba waendelee na kufanya usafi na hata kuwahamasisha watu wengine kuwa mabalozi wa mazingira ili kufikia malengo waliyojiwekea katika manispaa ya Ilala.
Baadhi ya wadau wa mazingira waliofika kwenye zoezi la usafi katika wiki ya Mazingira lililoendeshwa na kampuni ya Green Waste Pro Ltd wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Mstahiki Omary Kumbilamoto akizungumza jambo kwa wadau mbalimbali waliokuja kujumuika katika zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Agha Khan katika wiki ya mazingira.
Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste ProLtd, Abdallah Mbena akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa kampuni hiyo katika zoezi la kufanya usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya Kivukoni eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira.
Wafanyakazi wa Manispaa ya Ilala pamoja na wafanyakazi wa Green Waste Pro Ltd wakiendelea kufanya usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya Kivukoni eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira. Mwenye shati nyeupe ni Meneja Msaidizi wa kampuni Green WastePro ltd, Erick Mark.
Baadhi ya wadau wa mazungira wakifanya zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan kata ya Kivukoni ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira huku akishirikiana na viongozi wa kampuni iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd pamoja na wafanyakazi wa manispaa ya Ilala.

Baadhi ya uchafu ukiwa kwenye mifuko yake mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan kata ya Kivukoni ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira huku akishirikiana na viongozi wa kampuni iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd pamoja na wafanyakazi wa manispaa ya Ilala.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Green WastePro Ltd mara baada ya kumaliza kufanya usafi kwenye fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan kata ya Kivukoni ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira.

Tuesday, 13 September 2016

MUWSA WASAFISHA MIFEREJI YA MAJI TAKA KITUO KIKUU CHA MABASI MJINI MOSHI

Tope zilizokuwa zimetuama katika mifereji ya kusafirisha maji taka katika kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi zikiondolewa.
Licha ya kuwepo na kampuni iliyopewa kandarasi ya usafi katika kituo kikuu cha mabasi cha mjini Moshi bado changamoto ya kuziba kwa mifereji ya kusafirisha maji taka imekuwepo .
Wafanyakazi wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) walishiriki kuzibua na kuondosha taka zote zilizokuwepo katika mifereji hiyo.
Kitengo cha maji taka cha Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi kilihusika zaidi kuhakikisha hakuna mfereji utakao kuwa umebaki na taka.
Taka ngumu zote ziliondolewa katika mifereji hiyo.
Baadhi ya wafanyabiashara katika kituo hicho kikuu cha mabasi walijitokeza pia katika kusaidia kufanya usafi .
Wafanyakazi wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukamilisha zoezi la usafi katika kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA