Monday, 24 October 2022

FAIDA ZA KUTUMIA JUICE AU CHAI YA TANGAWIZI





Katika miaka 500 iliyopita tangawizi ilianza kutumika mashariki ya mbali, kama vile China na India wakitumia kwa kutibu maradhi mbali mbali.

Katika hili zao la tangawizi kuna vyanzo vya:
Mangenisium
Mangnese
Potasium
Copper
Vitamini B6

Hii ikiwa katika mwili wa binaadamu ikiwa ni pamoja na ugunduzi wa wataalamu kutengeneza tangawizi ni tiba tosha kwa magonjwa ya ngozi.


Hili hapa kwenye picha ni zao la tangawizi kama linavyoonyesha likiwa bado kusagwa.

Faida za kutumia tangawizi:

Husaidia kupunguza kama si kuondoa kichefuchefu ni nzuri haswa kwa wale wnawake wenye 
mimba changa ambao husumbuliwa kutapika.

-Husaidia wale wenye matatizo ya gauti yaani sehemu ya viungo kuuma na kusikia maumivu makali kupata ahueni, pia husaidia kusambaza damu kwenye mwili kwa haraka zaidi.

-Husaida msago wa chakula kwa haraka zaidi kwa kuchanganya na tindikali tumboni.

-Husaidia kwa wale wanaosafiri baharini ikiwa na machafuko kuzuia kutapika,kwa kutumia nusu saa kabla ya kusafiri na boti.

-Husaidi kupigana na kukinga kansaa ya kizazi.

-Tangawizi husaidia kupunguz maumivu mwilini

-Husaidia kutoganda kwa damu mwilini

-Wataalamu wamegundua tangawizi ni dawa tosha ya presha kuliko kitunguu swaumu.

Husaidi kuponya fluu kwani chai ya tangawizi ni salama



Hizi ndizo kazi za Tangawizi kama tiba ya afya yako


Tangawizi ina umuhimu mkubwa kwa afya ya binadamu. Sana sana tangawizi 
hutumika kama kiungo katika mapishi. Manufaa yake kiafya ni kama ifuatavyo.

Tumbo:
 
Tangawizi inatumika kutuliza maumivu ya tumbo, yanayotokana na matatizo ya 
usagaji chakula, kuharisha, kuvimbiwa, n.k. Inapotumiwa katika chakula tangawizi husaidia usagaji chakula. Aidha tangawizi humuongezea mtu hamu ya kula.
Kichefuchefu na Kutapika:
 Utafiti unaonyesha kuwa tangawizi ni tiba mufti kwa matatizo haya. Aidha huweza kutumiwa kupunguza tapishi inayotokana na uja uzito.

Matatizo ya Moyo:
 Tangawizi huimarisha moyo wa binadamu na kumwepushia maradhi ya moyo. Hii ni kwa kuwa inapunguza kiwango cha mafuta mwilini.

Matatizo ya Kupumua:
 
Huondoa homa ya mafua, hutumika kutibu pumu, na pia kufungua mfumo wa upumuaji hasa inapotumika pamoja na asali.

Maumivu:
 Huondoa maumivu ya misuli, kichwa, na shinikizo la mawazo, kisunzi, na kukosa umakini.

Maumivu ya Hedhi:
 Hupunguza maumivu ya wakati wa hedhi.

Malaria:
 Husaidi kutibu Malaria na Homa ya Manjano.

Nguvu za Kiume:
 T
angawizi husaidia kuongeza nguvu za kiume kwa kutibu tatizo la mwanamume kutoa shahawa haraka.

Figo:
 
Inaaminika kuwa tangawizi inatibu tatizo la vijiwe vya kwenye figo.

Nywele:
 
Aidha hutumiwa kutunza nywele, kwa kuwa huondoa uyabisi (Dandruff.)

Saratani:
 
Hutumiwa na wataalamu wa kimatibabu katika tiba ya saratani.
-mtandao

  1 comment:

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA