Friday, 15 September 2023
Monday, 22 November 2021
RAIS SAMIA ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WAPYA 118
18:01 |
No Comments |
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mh.Samia Suluhu Hassan ametunuku kamisheni kwa maafisa wanafunzi katika chuo Cha mafunzo ya kijeshi Monduli mkoani Arusha
Maafisa hao wapya ni kundi la 02/18-Shahada ya Sayansi ya kijeshi (BMS)idadi 61 ambao wamepata mafunzo miaka mitatu na kuhitimu shahada ya Sayansi ya kijeshi pamoja na kundi la 08/18 Jeshi la Anga idadi 56 waliopata mafunzo katika shule ya Anga ya kijeshi hapa Nchini
Aidha katika wahitmu hao kuna marubani wa ndegevita,Marubani na Wahandisi Ndege huku waliopata kamisheni jumla yao ni 118,kati yao wanaume 99 na wanawake 19
Zoezi la kutunuku kamisheni kwa maafisa hao lilifanyika kwa mara ya kwanza na Rais na Amir Jeshi Mkuu tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu na ni mara ya pili kutunuku kamisheni ambapo mara ya kwanza ilikuwa tarehe 17 April 2021 Ikulu jijini Dodoma
Kabla ya kutunuku kamisheni,Rais Mama Samia amekagua Gwaride lililoandaliwa na maafisa wanafunzi hao na baadae aligawa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kwa kila kundi
Wakati huo huo Rais Mama Samia alitunuku shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi kwa maafisa wapya 61
Mafunzo ya shahada hiyo yaliendeshwa katika chuo Cha mafunzo ya kijeshi Monduli kwa kushirikiana na chuo cha Uhasibu njiro (IAA)
Sherehe hizo zilihudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwepo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ,wawakilishi wa nchi rafiki ,makamanda,walezi na wawazi wa maafisa wapya.
Picha na Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi kundi la 02/18 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika sherehe zilizofanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (Tanzania Millitary Academy - TMA) mkoani Arusha leo tarehe 22 Novemba 2021.

.jpg)
.jpg)
.jpg)