Jackline Wolper na Irene Uwoya wamaliza bifu lao na kupatana
Ule ugomvi uliokuwepo kwa takribani miaka miwili kati ya mastaa wakubwa na warembo Jackline Wolper na Irene Uwoya hatimaye umefikia tamati baada ya kupatanishwa juzi.
Wawili hao walidaiwa kuingia katika beef zito baada ya Uwoya kumsema Wolper vibaya kwenye media ambapo pia aliwahi kukaririwa na gazeti moja akiwa jijini Arusha akisema kuwa Wolper amemroga ili amshushe kwenye sanaa na yeye(Wolper) kuwa juu kisanaa kitu ambacho kilidaiwa kumuudhi sana Wolper.
na wananchi Blg
0 comments:
Post a Comment