Friday, 28 March 2014

RAIS KIKWETE ATOA MSIMAMO ENDAPO BUNGE LITAVUNJIKA....ASEMA KATIBA YA ZAMANI ITAENDELEA KUTUMIKA....ADAI NI WAJIBU WAKE KUWAELEZA WANANCHI UKWELI



Posted by william Malecela on 3:12 PM with No comments

RAIS Jakaya Kikwete amesema kama mchakato wa upatikanaji Katiba Mpya utakwama kwa namna yoyote, Katiba iliyopo sasa itafanyiwa marekebisho na kuendelea kutumika.
 
Alisema kama Kiongozi Mkuu wa Serikali ni wajibu wake kuwaeleza ukweli wananchi kama alivyowasilisha hotuba yake kwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba Mjini Dodoma, kuhusu hatari ya muundo wa Serikali tatu ambayo ndiyo iliyopendekezwa kwenye rasimu.
 
Rais Kikwete aliyasema hayo juzi wakati akijibu risala ya wazee wa Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga, waliofanya mazungumzo naye nyumbani kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Subira Mgalu, akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani humo.
 
Alisema Katiba ni jambo muhimu katika nchi na itatumika kwa miaka 50 ijayo hivyo ni wajibu wa wajumbe kupitisha Katiba bora ambayo utekelezwaji wake hautakwama baada ya kupitishwa.
 
Aliongeza kuwa, pamoja na kasoro zilizopo kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba, bado hakuwasemea wajumbe wa Bunge hilo katika hotuba yake aliyoitoa bungeni bali aliamua kuweka bayana kasoro husika ili wajumbe waamue wenyewe muundo wa Serikali mbili au tatu kwani uamuzi ni wao.
na wananchi blg
 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA