PICHA ZA GARI LILILOTUMBUKIA MTONI USIKU WA KUAMKIA JUMAMOSI BONGO
|
Ajali hii imetokea usiku wa kuamkia jana jumamosi katika daraja la mto Kanoni barabara iendayo Bandarini kwenye manispaa ya Bukoba, ambapo Gari aina ya Toyota yenye namba za usajili T 910 CTC, lime tumbukia ndani ya mto Kanoni ambalo mmiliki wake hajafahamika
Japo katika eneo la tukio mwananchi mmoja alisikika akisema ni mali ya Askari Polisi ambaye hakumtaja jina, Mtandao huu ulifika kwenye kituo cha Polisi kujiridhisha na tulikutana na Bw Magayane ambae ni msaidizi katika kitengo cha Usalama Barabarani alikiri kuwa na Tarifa za ajali hiyo na kusibitisha kuwa hakuna aliyeumia, na nilipotaka kujua mmiliki wa Gari hili alisema hawamjui wapo katika jitihada za kumtambua.
Baadhi ya watu wakiangalia ajari hiyo kwa taharuki kubwa!
Mwendo kasi, ulevi, kuongea na simu ni hatari unapoendesha gari kuwa makini.
PICHA NA JAMCO BLOG
0 comments:
Post a Comment