FID Q AFUNGUKA>>>SINA BIFU LOLOTE NA WEUSI
Fid Q alipoulizwa
ilikuaje akajibu ‘Zile ni style za show tu mtu anakuja anasema sisi
tufanye kama suprise lakini sio kwamba walikua hawataki, mimi na WEUSI
tuko poa’
Soudy Brown: Mbona watu wanasema tuzo ulizoshinda ndio zimeleta matatizo?
Fid Q:
Hapana na sidhani kama zinaweza kuleta matatizo kwa sababu nina uhakika
hata WEUSI wanajua tuzo niliyopewa ninastahili labda kama wao sio
hiphop.. hatuna matatizo, hata jana baada ya kuchukua tuzo nilikua
kwenye viwanja tofautitofauti na Joh Makini.
Fid Q: Hakujawahi kuwa na tatizo isipokua mashabiki ndio waliwahi kuhisi kuna matatizo, wakati mwingine inabidi uache fans wawe fans.
Baada
ya hayo maneno ya Fid Q Soudy Brown alimpata msemaji wa WEUSI ambae ni
rapper Nikki wa II aliesema ‘hakuna ukweli kwamba tumekataa
kutambulishwa na Fid Q, kama umefatilia show zetu nyingi huwa hatuna
utaratibu wa kutambulishwa kwa sababu huwa imezoeleka kila mtu akiingia
anatambulishwa, ni kitu ambacho kimezoeleka sana, hata Fiesta yenyewe
huwa tunatokea tu bila kutambulishwa’
Kwa kumalizia Nikki wa II amesema labda tofauti iliyopo kati yake na Fid Q ni rasta au majina ila wako sawa na mtu yeyote.
Soudy Brown: Mlipatana lini?
Nikki wa II: ‘Kwani tuliwahi kugombana?’
0 comments:
Post a Comment