HABARI KUHUSU BOMU LILILO LIPUKA KATIKA KANISA LA KKKT MWANZA. NA KUMJERUHI MHUDUMU WA KANISA HILO
Picha ya kanisa kutoka maktaba |
MHUDUMU wa
nyumba ya kupumzikia wageni wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki ya
Ziwa Victoria, jijijini hapa, amejeruhiwa vibaya baada ya kulipukiwa na
bomu lililokuwa limewekwa kwenye korido la nyumba hiyo.
Tukio
hilo lilitokea jana (Jumatatu), kati ya saa 1:45 na saa 2:20 usiku,
katika eneo la Makongoro wilayani Ilemela wakati mhudumu huyo
Bernadetha Alfred (25) alipofungua kifurushi cha mzigo alichodhani
kimesahaulika kwenye eneo hilo, kabla ya kumlipukia.
Kwa
mujibu wa Katibu wa Dayosisi hiyo, Mollel Rogart, kifurushi hicho
kilichokuwa kwenye mfuko mweusi wa nailoni, kilikuwa juu ya kreti (tupu)
za soda, karibu na eneo la kulia chakula lililopo katika nyumba hiyo.
“Ule
mfuko ulikaa pale siku tatu ndiyo usiku huo mhudumu wetu akakichukua
kukiangalia akidhani ni mzigo wa mtu umesahaulika.” Alieleza Katibu huyo
na kudai kuwa kifurushi hicho kilimlipukia mara tu alipokifungua na
kujeruhi vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili.
“Bernadetha
kajeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo miguuni na usoni na
siwezi kusema kwamba chanzo cha mlipuko huo ni mambo ya kidini japo
ulinzi wetu haukuwa mkali kiasi cha kudhibiti watu walioingia na vitu.”
Alisema
Kamanda
wa polisi mkoani Mwanza, Valentino Mlowola akithibitisha tukio hilo,
alisema kwamba uchunguzi wa awali uliofanywa na kikosi maalum kutoka Dar
es salaam umebaini kuwa bomu hilo limetengenezwa kienyeji.
“Bado
tunaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili tubaini ni nani kafanya ili
kama ni mtu au kikundi kimehusika tuchukue hatua haraka. Natoa wito kwa
wananchi kutochukua vitu ambavyo hawa uhakika navyo, wanapoona vitu vya
aina hiyo, watoe taarifa kwetu.” Alisema Kamanda Mulowola.
Mlowola
alieleza kuwa, Bernadetha aliyejeruhiwa vibaya katika sehemu mbalimbali
za mwili, alikimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya Bugando ambako
anaendelea na matibabu.
Kamanda
huyo alieleza kwamba, mabomu (yakiwemo ya kienyeji) yako katika mifumo
mbalimbali hivyo wananchi hususan wahudumu wa sehemu za mikusanyiko wawe
na tahadhari na vitu vinavyoonekana kusahaulika na wasisite kuwajulisha
polisi vinapoonekana hivyo.
Mlipuko
huo uliozusha hofu kwa waumini mbalimbali wakiwemo wa Kanisa hilo,
umetokea ikiwa ni wiki moja baada ya maadhimisho ya ‘Huduma ya Mtoto’
kwa makanisa mbalimbali ya Kikristu jijini hapa yaliyofanyika kwenye
kanisa hilo, yakitanguliwa na maandamano kutoka uwanja wa furahisha hadi
KKKT.
0 comments:
Post a Comment