JAMAA ANASWA NA MADINI FEKI.. ANGALIA PICHA
Kijana aliyefahamika kwa jina la Samson Ntemi aliyetuhumiwa kwa utapeli wa madini bandia
MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Samson
Ntemi (44) mkazi wa Msingwi, Wilaya ya Magu mkoani Mwanza amenaswa na
Polisi wakati akifanya jaribio la utapeli wa madini feki huko
Kijitonyama jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kwa mujibu wa chanzo
makini, mtu huyo alianza harakati za utapeli wake kwa kumpigia simu
mfanyabiashara mmoja wa magari akimweleza kuhusu nia yake ya kununua
gari aina ya Canter kutoka kwake kwa kiasi cha shilingi milioni 32.
Chanzo kilisema kufuatia simu mfululizo za
mtu huyo, mfanyabiashara huyo alipata hofu na kuhisi huenda alikuwa ni
tapeli, hivyo kuweka mtego na kumtaka wakutane Mwananyamala kwa ajili ya
kufanya biashara hiyo. Lakini hata hivyo, walipokutana tapeli huyo
alimtaka mfanyabiashara huyo kuongozana naye hadi Kurasini, akidai ndipo
alipokuwa mteja mwenye kulihitaji gari hilo.
“Nilishangaa jamaa akinibadilishia kauli akidai anayetaka gari ni bosi wake siyo yeye.
Nilipomhoji vizuri akaniambia yeye ni
mfanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, Ifakara, mkoani Morogoro
aliyefika Dar kutafuta soko huku akionesha kutolijua vizuri Jiji la
Dar,” chanzo chetu kilimnukuu mfanyabiashara huyo akisema.
Inadaiwa kuwa tapeli huyo alimwonyesha
mfanyabiashara huyo madini hayo yenye thamani ya mamilioni ya shilingi
na kumtaka anunue. Baada ya kuyaona na kugundua kuwa ni feki, alimtaka
tapeli huyo kuandamana naye hadi benki maeneo ya Kijitonyama ili
amkabidhi.
Wakiwa njiani, mfanyabiashara huyo
aliwasiliana na Polisi wa Kituo Kidogo cha Mabatini, Kijitonyama ambao
walikuja eneo la tukio na kumkamata tapeli huyo, aliyekiri mbele ya
askari kuwa alishawahi kufanya wizi huo katika miji ya Tarime, Arusha na
Shinyanga.
NA MATUKIO NA VIJANA
0 comments:
Post a Comment