TAIFA STARS, MALAWI UWANJANI DAR
Taifa
Stars na Malawi (Flames) zinapambana leo katika mechi ya kirafiki ya
kimataifa itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11
kamili jioni.
Malawi
tayari ipo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi hiyo wakati Taifa
Stars iliyopiga kambi yake Tukuyu mkoani Mbeya inawasili jijini Dar es
Salaam leo saa 4 asubuhi kwa ndege ya Air Tanzania.
Kiingilio
katika mechi hiyo kitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa,
bluu na kijani. Kwa upande wa VIP B na C kiingilio kitakuwa sh. 10,000
wakati kwa VIP A itakuwa ni sh. 20,000.
Hiyo
itakuwa ni mechi ya mwisho ya majaribio kwa Taifa Stars inayodhaminiwa
na Kilimanjaro Premium Lager kabla ya kwenda jijini Harare kwa ajili ya
mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika dhidi ya Zimbabwe (Mighty
Warriors).
Malawi
(Flames) inayonolewa na mchezaji wake wa zamani Young Chidmozi nayo
itakuwa inacheza mechi ya mwisho ya majaribio kabla ya kwenda N’djamena
kuikabili Chad.
U15 TANZANIA NG’ARING’ARI AYG
Tanzania
imeendelea kung’ang’ara kwenye Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) kwa
upande wa mpira wa miguu kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 baada
ya jana (Mei 25 mwaka huu) kuichapa Swaziland mabao 3-0.
Mabao ya
Tanzania katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Gaborone,
Botswana yalifungwa na Amani Ally dakika ya sita, Nasson Chanuka dakika
ya 32 wakati Amos Kennedy alikamilisha ushindi huo kwa bao la dakika ya
53.
Katika
mechi yake ya kwanza, Tanzania ilitoka sare ya bao 1-1 na Mali na
baadaye kuwafunga wenyeji Botswana mabao 2-0. Mechi za michuano hiyo
zinaoneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha SuperSport cha
Afrika Kusini.
Tanzania
itacheza mechi yake ya nne kesho (Mei 27 mwaka huu) dhidi ya Nigeria
wakati mechi ya mwisho itafanyika Mei 29 mwaka huu dhidi ya Afrika
Kusini.
KOZI ZA UKOCHA LESENI A, B KUFANYIKA JUNI
Kocha a
ukocha wa mpira wa miguu kwa ajili ya Leseni A na B zinazotambuliwa na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) zitafanyika jijini Dar es
Salaam kuanzia Juni 2 mwaka huu.
Ada kwa
kozi ya Leseni A itakayoanza Julai 21 hadi 26 mwaka huu ni sh. 300,000
wakati ile ya Leseni B itakayofanyika kuanzia Juni 2 hadi 15 mwaka huu
ni sh. 200,000. Maombi ya kushiriki kozi hizo yatumwe kwa Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakati kwa upande wa
Zanzibar yatumwe kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar
(ZFA) kabla ya Mei 31 mwaka huu.
Washiriki
ambao watajitegemea kwa chakula watalipa ada hizo wakati wa usajili
utakaofanyika Juni 1 mwaka huu kwa upande wa Leseni B na Leseni A
watalipa Julai 20 mwaka huu vilevile wakati wa usajili.
TFF
itatoa malazi kwa washiriki kwenye hoteli yake iliyopo Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume wakati wakufunzi wa kozi hizo ni Sunday Kayuni na
Salum Madadi ambao wanatambuliwa na CAF. Pia CAF baadaye itatuma
Mkufunzi atakayetunga na kusimamia mitihani hiyo.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment